loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mahakama yaamuru Wema akamatwe

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, imetoa hati ya kukamatwa kwa msanii wa fi lamu nchini, Wema Sepetu kutokana na kuruka dhamana.

Hatua hiyo imekuja baada ya Wakili wa Serikali, Sylvia Mitanto kudai mbele ya Hakimu Mkazi, Maira Kasonde kuwa kesi hiyo imekuja kwa ajili ya kusikilizwa. Pia alidai kuwa mshitakiwa hayupo mahakamani na hakuna taarifa yoyote inayohusiana na kutofika kwake.

Baada ya kueleza hayo,wakili wa utetezi, Reuben Simwanza alidai kuwa mshitakiwa Wema alifika mahakamani hapo lakini akaumwa ghafla, hivyo alishindwa kuingia kwenye chumba cha mahakama. Hakimu Kasonde aliamuru kutolewa kwa hati ya kumkamata Wema kwa sababu kama alifika mahakamani kwanini alishindwa kuingia mahakamani hapo.

Wema anakabiliwa na mashitaka ya kusambaza video ya ngono katika mtandao wake wa kijamii wa Instagram kupitia simu yake ya kiganjani. Anadaiwa kutenda kosa hilo kati ya Oktoba 15, 2018 katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam, picha ambazo inadaiwa kuwa haina maudhui.

MABINGWA wa kihistoria, Yanga wametua Musoma, Mara, huku kocha wao ...

foto
Mwandishi: Francisca Emmanuel

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi