loader
Picha

Zimamoto yaanza kunoa makali

UONGOZI wa timu ya soka ya Zimamoto inayoshiriki Ligi Kuu ya Zanzibar unatarajia kuanza mazoezi Juni 25 mwaka huu.

Timu hiyo ambayo ilikuwa mapumziko kupisha mfungo wa mwezi wa Ramadhani itaanza mazoezi hayo kwa ajili ya kujiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu ya Zanzibar inayotarajiwa kuanza Agosti 25 mwaka huu.

Katibu wa Michezo wa Kikosi hicho, Ali Ussi Jongo akizungumza na mwandishi wa habari hizi ofisini kwake Maisara mjini hapa, alisema kuwa mazoezi wanayoanza ni kwa ajili ya kuwaangalia wachezaji wake waliomo kwenye vikosi uwezo wao. Alifahamisha kwamba kwa mujibu wa ratiba ya mwalimu wa mazoezi rasmi wataanza Julai mosi mwaka huu, lakini Juni 25 wataanza kidogokidogo ili kujua uwezo wa wachezaji walionao.

“Mazoezi rasmi tutaanza Julai mosi ila Juni 25 tutakayoanza ni kwa ajili ya kuangalia uwezo wa wachezaji tulionao kwenye kikosi”, alisema. Alisema, katika msimu huu wanajiandaa kuhakikisha timu inakuwa bora na kutoa ushindani kwenye ligi hiyo kama ambavyo vijana wake wanavyopambana kila mwaka.

Timu ya soka ya Zimamoto inashiriki Ligi Kuu ya Zanzibar ambapo katika msimu wa ligi uliopita ilishika nafasi ya tatu na kukosa nafasi ya kushiriki michuano ya kimataifa. Imeshiriki michuano ya kombe la Shirikisho Afrika misimu miwili mfululizo.

Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Dar es Salaam, Mhashamu ...

foto
Mwandishi: Mwajuma Juma, Zanzibar

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi