loader
Picha

Mourinho adaiwa kurejea Chelsea

JOSE Mourinho anatarajiwa kurejea Chelsea msimu huu, kwa mujibu wa taarifa. Bosi wa sasa wa Chelsea, Maurizio Sarri anatarajiwa kuondoka klabuni hapo na kujiunga na mabingwa wa Italia, Juventus.

Kocha huyo mwenye umri wa miaka 60 amekubali mkataba wa miaka mitatu Juve. Na taarifa za The Sun zinasema kwamba Jose Mourinho, ambaye alifukuzwa mara mbili na Chelsea, anapewa nafasi kubwa ya kurejea.

Gwiji wa klabu hiyo Frank Lampard bado anabakiwa kuwa ndiye anayepewa nafasi kubwa kama kocha wa Blues, lakini taarifa za kurejea kwa Mourinho huenda zikawashtua mashabiki wa Stamford Bridge.

Taarifa zimesema Chelsea inataka kuajiri kocha mwenye uzoefu. Mreno huyo amekuwa hana kazi tangu alipofukuzwa Manchester United Desemba mwaka jana, baada ya kutoelewana na wachezaji, jambo lililosababisha kupata matokeo mabaya. Uchunguzi wa Express Sport umebaini kuwa Chelsea ina orodha ya makocha sita wanaowania nafasi ya Sarri.

Kocha wa Wolves Nuno Espirito Santo, Javi Gracia wa Watford na Lampard wote wapo kwenye orodha hiyo pamoja na kocha wa zamani wa Juve, Massimiliano Allegri. Kocha wa Ajax, Erik ten Haag na kocha msaidizi wa zamani wa Blues, Steve Holland nao wanazungumzwa kuchukua nafasi hiyo. Machi mwaka huu, Mourinho alizungumzia mipango yake ya kurejea kwenye ukocha msimu huu.

Alisema: “Nilichonacho kwenye fikra zangu nitarudi kwenye msimu ujao (huu), Juni kwa klabu mpya kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya. “Najua vizuri nisichokitaka.” “Ndio sababu nimesema tayari nina ofa tatu au nne tofauti.” “Na najua ninachokitaka kwamba ni klabu ipi hasa, kwa kazi yangu najua nini nataka.” Alipokuwa Chelsea, Mourinho alishinda mataji matatu ya Ligi Kuu, matatu ya kombe la ligi na FA.

HATUA ya makundi ya Ligi ya ...

foto
Mwandishi: LONDON, England

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi