loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mwananyamala, Temeke na Amana zafungiwa CT-Scan

SERIKALI imeanza kufunga mashine za CT-Scan katika Hospitali za Rufaa za Mwananyamala, Temeke na Amana mkoani Dar es Salaam.

Kauli hiyo aliitoa Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Faustine Ndugulile wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu, Mariam Kisangi (CCM) aliyehoji serikali ina mpango gani wa kupeleka vipimo vya MRI katika Hospitali za Amana, Temeke na Mwananyamala.

Dk Ndugulile alisema kutokana na mwongozo uliokuwepo huduma za CTScan na MRI hazikuwepo kwenye hospitali za rufaa za mikoa zikiwemo Amana, Temeke na Mwananyamala.

Hata hivyo, alisema kutokana na mabadiliko ya kiuchumi na uhitaji wa huduma hizo kwa wananchi, wizara ya afya ilifanya mabadiliko ya mwongozo kwa kutengeneza mwongozo wa vifaa vya radiolojia nchini wa mwaka 2018. “Pamoja na mengine huduma za CT-Scan sasa zinapatikana katika ngazi ya hospitali ya Rufaa za mikoa na huduma za MRI zinapatikana katika ngazi za hospitali za rufaa za kanda na taifa,” alisema.

Katika swali la nyongeza la Kisangi, alitaka kujua ni lini mashine hizo zitafungwa katika hospitali hizo ili kupunguza msongamano katika Hospitali ya Taifa Muhimbili. Pia alitaka kujua ni lini serikali itafunga mashine hizo katika Hospitali ya Kijibweni inayotumika kama hospitali ya wilaya ya Kigamboni na Sinza Palestina ya Wilaya ya Ubungo ili kupunguza msongamano wa wananchi kwenda kutibiwa Muhimbili.

Akijibu maswali hayo, Dk Ndugulile alisema, mahitaji ya mashine za CT-Scan na MRI ni muhimu katika kusaidia wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam na ndio maana serikali imezifunga mashine hizo katika kanda na taifa na sasa imezifunga katika hospitali za rufaa za mikoa ili kupunguza msongamano katika Hospitali ya Rufaa Muhimbili.

Waziri huyo alisema mkakati huo unalenga kupanua wigo wa huduma za afya katika maeneo mengine ili kupunguza msongamano katika hospitali ya Muhimbili ndio maana katika hospitali ya Kijibweni inafungwa mashine ya MRI kigamboni kwa lengo hilo.

KAYA zilizobainika kuwa na historia ya kutochukua mara ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi