loader
Picha

Chuo kikuu China chafundisha shahada ya Kiswahili

CHUO Kikuu cha Taaluma za Lugha za Kimataifa cha Shanghai (SISU) kilichopo Mashariki mwa China, kimeanzisha kozi ya shahada ya kwanza ya Kiswahili, ikiwa ni lugha pekee kutoka barani Afrika.

Ndicho chuo cha kwanza katika ukanda huo kufundisha Kiswahili, hivyo kikifanya kiwe na masomo saba ya lugha za kigeni.

Akizungumza katika kampasi kuu ya chuo hicho jijini Shanghai hivi karibuni, Mkuu wa Idara ya Kiswahili katika Shule Kuu ya Lugha za Asia na Afrika, Ma Jun ambaye alipikwa kukijua vyema Kiswahili katika Taasisi ya Taaluma ya Kiswahili (TATAKI) ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa takribani mwaka mmoja na nusu, alisema Kiswahili kina umuhimu wa pekee ndiyo maana imeanzishwa kozi maalumu ya Kiswahili katika mwaka huu wa masomo.

Alisema kozi hiyo ina wanafunzi kumi ambao wapo katika mwaka wa kwanza na kwamba wanatarajia kupokea wanafunzi wengi zaidi katika siku za usoni.

“Wanafunzi tulionao wote ni raia wa China. Lengo ni kuwafanya wazijue lugha za kimataifa kwa ufasaha na kuweza kurahisisha mawasiliano na mtangamano. Tumeona Kiswahili kinakua kwa kasi, nasi tumeona tusipitwe. Mbali ya Kiswahili wanafunzi hawa wanasoma pia juu ya uchumi, diplomasia, siasa, habari, utamaduni, na Kiingereza.

“Hawa wakihitimu baada ya miaka minne, tuna uhakika wataendelea kukuza Kiswahili katika sehemu nyingine hasa vyuoni. Usishangae kuona miaka michache ijayo Kiswahili kinapata umaarufu mkubwa hapa China,” alisema Ma anayezungumza na kuandika vizuri kwa lugha ya Kiswahili.

Mbali ya Kiswahili lugha nyingine za kigeni zinazofundishwa SISU ni pamoja na Kiarabu, Ki-vietnam, Ki-Indonesia, Ki-Malay (Malaysia), Kikorea na Kihindi.

Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Dar es Salaam, Mhashamu ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu aliyekuwa Shanghai, China

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi