loader
Picha

Majaliwa akaribisha wawekezaji kutoka Rwanda

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amewakaribisha wawekezaji kutoka nchini Rwanda waje wawekeze katika sekta mbali mbali na kwamba serikali itawapa ushirikiano wa kutosha.

Aliyasema hayo jana alipokutana na kufanya mazungumzo na Spika wa Bunge la Rwanda, Donatille Mukabalisa, ofisini kwake bungeni jijini Dodoma.

Alisema serikali ipo tayari kuwapokea wawekezaji kutoka katika nchi hiyo ili waje kuwekeza katika sekta mbali mbali zikiwemo za viwanda, kilimo, madini na utalii.

Kadhalika, Waziri Mkuu amesema Tanzania na Rwanda ni nchi zenye uhusiano mzuri, hivyo amemhakikishia Spika Mukabalisa kwamba serikali itaimarisha uhusiano huo.

Aidha, Waziri Mkuu amesema serikali inatekeleza mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) ambao unatarajiwa kusaidia katika usafirishaji wa mizigo kwenda hadi nchini Rwanda.

Spika Mukabalisa ameishukuru Serikali ya Tanzania kwa ushirikiano mkubwa inaoutoa kwa Serikali ya Rwanda, hivyo amemhakikishia Waziri Mkuu kwamba watauendeleza.

Spika huyo amesema ushirikiano wa Tanzania na Rwanda ni muhimu katika uchumi kwa kuwa wanatumia bandari ya Dar es Salaam katika kusafirisha asilimia kubwa ya mizigo yao.

Alisema wananchi nao wanatakiwa wawe na ushirikiano katika nyanja mbalimbali kama za kibiashara. Ametumia fursa hiyo kuwakaribisha Watanzania wakawekeze nchini Rwanda.

SHIRIKA la Taifa la Biashara (ZSTC) limesema ni makosa kwa ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Maalumu, Dodoma

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi