loader
Picha

Polisi atuhumiwa kumjaza mimba mwanafunzi

ASKARI wa Jeshi la Polisi mwenye namba H. 9946, Konstebo Daniel wa Kituo cha Polisi Wilaya ya Kyela mkoani Mbeya, anasakwa na Polisi baada ya kutoroka akituhumiwa kumpa ujauzito mwanafunzi.

Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Sebastian Mbuta ilieleza Mei 28, mwaka huu asubuhi, Konstebo Daniel alitakiwa kuingia kazini lakini hakuingia.

Mbuta alisema baada ya kufuatilia ilibainika askari huyo alitoroka baada ya kutuhumiwa kumpa ujauzito mwanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Kyela anayesoma kidato cha kwanza (jina limehifadhiwa).

Aliongeza kuwa Jeshi la Polisi linaendelea na juhudi za kumtafuta askari huyo ili hatua za kinidhamu zichukuliwe dhidi yake, ikiwa ni pamoja na kumfikisha katika vyombo vya sheria.

Wakati huo huo, Kaimu Kamanda huyo alisema abiria waliokuwa wakisafiri na basi lenye namba za usajili T489 AUG, Scania mali ya Kampuni ya Sasebosa wamenusurika kufa baada ya gari kupata ajali.

Alisema ajali hiyo ilitokea Juni 10, mwaka huu saa 2:50 asubuhi eneo la Mlima Yasini lililopo Wilaya ya Chunya Mkoa wa Mbeya katika Barabara ya Chunya – Makongorosi.

Alisema basi hilo linalomilikiwa na Kampuni ya Sasebosa lilikuwa likiendeshwa na dereva Seleman Salehe (48), mkazi wa Tabora ambaye alitoroka baada ya ajali.

Alisema basi hilo baada ya kupinduka lilisababisha majeruhi kwa abiria Tila Mbeyu (70) mkulima na mkazi wa Dar es Salaam aliyeumia kiunoni na Jane Damiani (28), mkulima wa Kibaoni Chunya aliyeumia kifuani na mkono wa kushoto waliopelekwa kutibiwa Hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya.

Alisema chanzo cha ajali hiyo kinachunguzwa na Polisi inaendelea kumtafuta dereva huyo aliyetoroka.

Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Dar es Salaam, Mhashamu ...

foto
Mwandishi: Joachim Nyambo, Mbeya

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi