loader
Picha

Vyakula, dawa vyatajwa upungufu nguvu za kiume

Ofisa Lishe Mkoa wa Dar es Salaam, Janneth Mzava amesema, wanaume wanapaswa kubadili mfumo wa maisha na kupunguza msongo wa mawazo ili wawe na nguvu za kiume.

“Tunapozungumzia upungufu wa nguvu za kiume tunamanisha kukosa uwezo wa kufanya kabisa tendo la ndoa, uume kusimama muda mfupi baada ya tendo kuanza unasinyaa, na kushindwa kufika mwisho ama kuwahi kufika kileleni,” amesema Mzava.

“Suala hili ni mtambuka, linahitaji vyakula bora, wanaume wale makundi mchanganyiko ya chakula, wale mboga za majani kwa wingi, wanga, protein na pia wafanye mazoezi kuimarisha afya ya mbegu zao,” amesema.

Mfamasia wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na mtaalamu wa afya ya jamii, Edgar Basheka amekaririwa akisema dawa zinazotumika ili kumpa mwanaume uwezo wa kujamiana zina madhara makubwa na husababisha mwili wa mtumiaji kukosa mwelekeo.

Amesema kitendo cha vijana wa kiume kutumia dawa za kuongeza nguvu kunawanyima kujiamini wakiwa na wenza kwa kuhisi hawatamridhisha mpaka watakapotumia dawa hizo ndipo hali ya kujiamini inarejea.

Basheka amesema, madhara ya kutumia dawa yasiyofuata utaratibu, mtumiaji anaweza kuongeza dozi au kupunguza hivyo kuchelewesha kupona kwa tatizo au kuleta madhara makubwa zaidi.

Amesema kutumia dawa bila ya kufuata ushauri wa daktari, kunaongeza tatizo kwa kuwa dawa zinazotumika hazijafuata utaratibu, hakuna dawa isiyo na madhara.

“Kutumia dawa kunaleta usugu mwilini, mgonjwa angeweza kutibiwa kwa sh 20,000 sasa atatibiwa kwa sh. 800,000 kutokana na kujiongezea tatizo, mgonjwa afike kituo cha Afya apate ushauri na maelekezo maalumu, nawashauri vijana waache kutumia dawa hizo waende vituo vya Afya kwa ushauri", amesema.

“Dawa hutolewa kwa kufuata umri na uzito, sasa unatumiaje dawa usiyojua, wengi wanatumia dawa kwa kutofuata utaratibu, unapoenda kwa mtaalamu anajua akikupa dawa anafahamu kuna madhara unayapata ya muda mfupi lakini tatizo lako kubwa linapona, hivyo ni vyema waache kufanya hivyo”, amesisitiza.

Daktari wa magonjwa ya wanawake Hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala, Fabia Tumai amesema vijana hawajiamini ndio maana wanatumia dawa za kukuza maumbile ya uume wao.

Utafiti wa mwaka 2015 wa chuo kimoja London uliangalia urefu na upana wa uume kwa wanaume zaidi ya 15,000 duniani kote.

Kitaalamu uume unapaswa kuwa na inchi 5.1, sentimita 13 wakati unaposimama. Utafiti huo ulionyesha ni asilimia tano ya wanaume ndio wana uume wa urefu wa zaidi ya inchi 6.3, asilimia 0.14 wana uume mdogo kuliko kawaida, wa urefu wa chini ya inchi tatu ukisimama.

Kuhusu mzingo wa uume, ukubwa kwa mzunguko ambacho ni kipimo cha kukadiria upana wake, kiwango cha kawaida ni inchi 3.6 sawa na sentimita tisa ukiwa haujasimama na inchi 4.6 ukisimama.

NAIBU Waziri wa Maliasili na Utalii, Constantine Kanyasu ametoa maagizo ...

foto
Mwandishi: Vicky Kimaro

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi