loader
Picha

TTB kutangaza utalii miji 4 China

Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) imesema, itafanya misafara ya kutangaza utalii kwenye miji minne nchini China kati ya Juni 19 hadi Juni 26 mwaka huu.

Misafara hiyo itatembelea miji ya Beijing Juni 19, Shanghai Juni 21, Nanjig Juni 24 na Changsha Juni 26.

Mwenyekiti wa bodi TTB, Jaji Mstaafu Thomas Mihayo ameyasema hayo kwenye mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

“Tunafanya jitihada kuhakikisha tunavuna watalii wengi zaidi kutoka China hasa tukizingatia umuhimu wa soko la sekta ya utalii nchini,” amesema Jaji Mihayo.

Novemba 2018 TTB ilifanya ziara kwenye miji ya Beijing, Shanghai, Chengdu, Guangzhou na Hong Kong kutangaza vivutio vya utalii sanjari kuzitangaza safari za ndege za Air Tanzania.

Ziara hiyo inaelezwa kuzaa matunda ikiwa ni pamoja na watalii zaidi ya 300 kuja nchini Mei mwaka huu kutembelea vivutio vya utalii.

KITUO cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Kimesema, mkoa wa Pwani una ...

foto
Mwandishi: Na Janeth Mesomapya

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi