loader
Picha

Walinzi binafsi kusajiliwa upya TPSIS

TAASISI ya Huduma za Kuunganisha Walinzi Binafsi nchini (TPSIS) imezindua rasmi zoezi la usajili wa walinzi wote ambao hawapo katika mfumo rasmi wa kampuni za ulinzi nchini.

Chini ya mpango huo, TPSIS itashirikiana na Jeshi la Polisi katika kuwatambua, kuwakusanya na kuratibu mtandao wa walinzi binafsi, lengo kubaini matukio ya uhalifu kabla hayajatendeka.

Mkurugenzi Mtendaji wa TPSIS, Dk David Rwegoshora alisema hayo jana Dar es Salaam wakati akizindua huduma hiyo mpya nchini yenye lengo la kuleta mageuzi makubwa katika mfumo wa Taifa wa kuendeleza amani nchini. Dk Rwegoshora alisema chini ya mpango huo, walinzi binafsi ambao hawajasajiliwa kwenye makampuni ya ulinzi watapata fursa ya kujisajili na kuwawezesha wadau kama serikali, Jeshi la Polisi, mashule, makanisa, maduka na hata watu binafsi kujua mlinzi gani yupo wapi na mahitaji.

“Lengo letu ni kuwaunganisha watu wote wanaofanya kazi moja, lakini hawatambuani na kushirikiana. Tutafanya hivyo kwa kuwaingiza kwenye kanzidata yetu kwa mfumo na utaratibu wa usaili mzuri,” alisema Dk Rwegoshora. Alisema chini ya mfumo huo utakaofanyika kwa nchi nzima kupitia mifumo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama), usajili wa walinzi hao utazingatia sifa mbalimbali.

Alizitaja sifa hizo kuwa ni taarifa za kina za kila mhusika, lakini pia kuwapatia mafunzo maalumu ya kubaini matukio ya uhalifu kabla ya kutokea. “Kwa mfano katika tukio la ugaidi lililotokea Kenya hivi karibuni mlishuhudia mashuhuda wakisema magaidi walikuwa wakifika pale na wakati mwingine kushinda maeneo husika wakinywa kahawa na kupiga soga.

Tunataka kuwa na mfumo wa walinzi wanaoweza kutambua matukio kama haya kabla kwa kuwapa ujuzi wa hali ya juu,” alisema. Alisema utafiti uliofanyika karibuni ulibaini Tanzania kuwa na walinzi milioni mbili waliopo katika kampuni 400 za ulinzi, hali inayoashiria kuwepo idadi kubwa ya walinzi katika mfumo wa kampuni binafsi wanaotakiwa kusajiliwa ili waisaidie Polisi katika kupambana na uhalifu.

Mkurugenzi wa Tehama wa taasisi hiyo, Alphonce Christopher alisema teknolojia inayotumika kuwasajili itawezesha kutambuliwa mara moja mlinzi atakayefanya vitendo kinyume na maadili kwa kughushi taarifa.

BENKI ya NMB imezindua 'NMB Afya loan', ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi