loader
Picha

Kituo cha afya kikamilike ndani ya siku 18 - Waziri

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Selemani Jafo ametoa siku 18 kwa uongozi wa Jiji la Dodoma kuhakikisha kituo cha afya cha Mkonze kinakamilika kwa asilimia 100.

Jafo alitoa agizo hilo jana alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa kituo cha Mkonze ambacho ni miongoni mwa vituo vya kutolea huduma za afya 352, ambavyo viko kwenye mpango wa kuboresha huduma za afya katika Mamlaka za Serikali za Mitaa. Katika mpango huo kunafanyika ujenzi wa majengo sita ambayo ni chumba cha upasuaji, wodi ya mama na mtoto, maabara, nyumba ya mganga, chumba cha kufulia na kichomea taka.

Kutokana na kukuta kituo hakijakamilika Jafo alisema: “ Nimetoa maelekezo ifikapo Juni 30 mwaka huu kituo kile kiwe kimekamilika kwa asilimia 100. Nataka siku hizi chache zilizobakia Jiji la Dodoma lihakikishe linakamilisha kile kituo na mimi mwenyewe nitarudi tena kuangalia kama kituo kimekamilika.”

Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, Godwin Kunambi pamoja na kushukuru hatua ya serikali ya kutoa Sh milioni 400 kwa ajili ya ujenzi wa kituo hicho, jiji liliamua kujenga kituo chenye hadhi ya Sh milioni 500.

“Kwa vile Dodoma ni makao makuu ya nchi, sisi tuliona tujiongeze na tujenge kituo cha afya chenye hadhi ya Sh milioni 500 na kwa vile fedha za ziada takribani milioni 100 hazikuwa kwenye bajeti ya mwaka 2018/2019 tuliomba mapitio ya bajeti na Kamati ya fedha imesharuhusu fedha hizo zitumika. Kunambi alisema kituo hicho kitakamilika kwa muda ulioelezwa kwa sababu fedha ipo.

Katika hatua nyingine, Jafo ameridhishwa na maendeleo ya ujenzi wa barabara ya Kikuyu- Chidachi-Kinyambwe-Itega yenye urefu wa kilometa 6 inayojengwa kwa lami kwa thamani ya Sh bilioni 9 na Kampuni ya STECLO. Kwa upande wa barabara ya urefu wa kilometa 1.85 ya Martin Luther-Swaswa inajoyengwa kwa tahamani ya Sh bilioni 1.3, Jafo alimuagiza mkandarasi SKOL kuhakikisha anapeleka vifaa vingine ili kazi ya barabara ile ukamilike. “Tumekuta amepaki scaveter pembeni kwa sababu ya kuharibika, tunataka wakandarasi ambao wanapewa kazi wawe na uwezo wa vifaa, hivyo nataka mkandarasi yule kazi yake iendelee,” alisema.

BENKI ya NMB imezindua 'NMB Afya loan', ...

foto
Mwandishi: Anastazia Anyimike

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi