loader
Picha

Dk Saqware Makamu Rais Kampuni za Bima Afrika

KAMISHNA wa Bima, Dk Baghayo Saqware amechaguliwa kuwa Makamu wa Rais wa Umoja wa Wasimamizi wa Kampuni za Bima Afrika (AAISA) nafasi atakayoishika kwa kipindi cha miaka miwili.

Saqware alichaguliwa hivi karibuni katika Mkutano Mkuu wa umoja huo ambao umemchagua Boubacar Bah ambaye ni Mkurugenzi wa Bima nchini Guinea, kuendelea kuwa Rais kwa kipindi cha miaka mingine miwili.

Viongozi hao walichaguliwa na Mkutano Mkuu wa Pili uliofanyika juzi jijini Johannesburg, Afrika Kusini na kuhudhuriwa na wajumbe wake wote 24 kutoka nchi mbalimbali. Akizungumza na gazeti hili, Saqware alisema nafasi hiyo mpya itawezesha kufanya maboresho kwa sekta ya bima ambayo inaendelea kukua nchini na Afrika kwa ujumla.

Alisema bima katika Afrika ina mambo mengi yanayofanana ambayo yanahitaji nguvu ya pamoja kuyakabili. Mtafiti Mkuu kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Shughuli za Bima (TIRA), Dk Emmanuel Lupilya alimpongeza Saqware na kumtakia nguvu na mafanikio katika kipindi cha uongozi wake.

Lupilya ambaye aliongozana na Saqware katika mkutano huo, alisema kama nchi, panahitaji ubunifu wa maendeleo, ujasiri katika uongozi na mipango ya kimkakati itakayoleta mabadiliko na ubora zaidi kwa sekta ya bima. Dk Saqware alisema ameweka vipaumbele vyake ambavyo pia vitanufaisha Tanzania ikiwemo kuendeleza na kuhakikisha sekta inafikiwa, inaaminika, inategemewa na kuwa kiunganishi.

Katika mkutano huo, alishukuru wajumbe kumuamini na kumchagua kuwa Makamu Rais. Aliwahakikishia kuwa pamoja nao katika kuongoza umoja huo ambao Makao Makuu yake yako Yaoundé, Cameroon.

Malengo makuu ya umoja huo ni kuendeleza ushirikiano miongoni mwa mamlaka za usimamizi kusaidia nchi zao katika suala zima la maendeleo ya raslimali watu. Mengine ni kutengeneza jukwaa kwa ajili ya kuwa na viwango sawa vya sheria ya bima na mfumo wa usimamizi katika bara.

Ajenda kuu ya mkutano ilihusu kufahamisha wasimamizi kuhusu maazimio yaliyopitishwa Machi 31 na Aprili Mosi, mwaka huu Casablanca nchini Morocco; kupitisha Katiba na Sheria Ndogo za chama, Kutoa taarifa ya hali ya fedha, Kufanya uchaguzi wa Rais na Makamu Rais. Kwa mujibu wa Katiba ya chama, Mkutano Mkuu ni chombo kikuu cha uongozi

BENKI ya NMB imezindua 'NMB Afya loan', ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi