loader
Picha

Uchaguzi serikali mitaa kutumia bilioni 82.97/

JUMLA ya Sh bilioni 82.97 zimetengwa kwa ajili ya kuendesha uchaguzi wa serikali za mtaa uliopangwa kufanywa baadaye mwaka huu. Hayo yamebainishwa jana bungeni na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi), Mwita Waitara (pichani).

Waitara alikuwa wakati akijibu swali la msingi la mbunge wa Mtambile, Masoud Abdalah Salim (CUF) aliyehoji mwaka huu ni wa uchaguzi serikali za mitaa na serikali ina mikakati gani. Waitara alisema serikali imekamilisha maandalizi ya kanuni za uchaguzi huo zitakazotumika kuendesha na zimetangazwa katika gazeti la serikali la Aprili 26, mwaka huu.

Waitara alisema serikali imeshahakiki maeneo ya utawala na kufanya mafunzo na mikutano kwa wadau wa uchaguzi huo na kwamba fedha sh bilioni 82.97 zimetengwa kwa ajili ya kuendesha uchaguzi huo huko pia ununuzi wa vifaa kwa ajili ya uchaguzi huo ukiendelea. “Uchaguzi wa serikali za mitaa utafanyika kwa ufanisi. Serikali tumekamilisha kanuni za uchaguzi na pesa Sh bilioni 82.97 zimetengwa kwa ajili ya kuuendesha,” alisema Waitara.

Mapema Aprili mwaka huu bungeni, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati akiwasilisha mapitio na mwelekeo wa kazi za serikali kwa mwaka ujao wa fedha alisema uchaguzi huo wa utafanywa Oktoba mwaka huu halmashauri 185. Uchaguzi huo ni wa sita kufanywa nchini tangu kuanza mfumo wa vyama vingi mwaka 1992.

Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Dar es Salaam, Mhashamu ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi