loader
Picha

Kiingereza kuendelea kufundishia sekondari

LUGHA ya Kiingereza itaendelea kutumika kufundishia na kujifunzia katika ngazi ya elimu ya sekondari, vyuo vya kati na vyuo vikuu nchini kwa sababu ya umuhimu wake kitaifa na kimataifa sambamba na kuwajengea ufahamu na umahiri wa wanafunzi katika lugha hiyo.

Bunge lilielezwa hayo jana na Waziri wa Elimu ,Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako wakati akijibu swali la msingi la mbunge wa Tabora Kaskazini, Almas Maige (CCM), aliyehoji ni nini kimetokea kwa serikali kutumia Kiswahili kama lugha ya kufundishia katika shule zake za msingi na sekondari nchini.

Akijibu swali hilo, Waziri Ndalichako alisema suala la matumizi ya lugha ya kufundishia na kujifunzia katika shule ni la kisheria, kama ambavyo sheria ya Elimu sura 353 inavyoeleza.

Alisema sheria hiyo inabainisha matumizi ya lugha mbili za kufundishia na kujifunzia ambazo ni Kiswahili na Kiingereza. Alisema kwa sasa lugha ya Kiswahili inatumika kufundishia ngazi ya Elimu ya awali na msingi, vyuo vya ualimu ngazi ya cheti na ufundi stadi.

Aidha lugha ya Kiingereza bado inatumika kufundishia na kujifunzia ngazi ya elimu ya sekondari, vyuo vya kati na vyuo vikuu kwa umuhimu wake kitaifa, kikanda na kimataifa.

“Bado serikali inatumia lugha ya Kiingereza kufundishia elimu ya sekondari vyuo vya kati na vyuo vikuu kwa umuhimu wake kuwajengea wanafunzi ufahamu na umahiri wa kutumia lugha hiyo,”alisema Waziri Ndalichako. Awali akijibu swali la mbunge wa Viti Maalumu, Munira Khatib (CCM) aliyehoji serikali ina mpango ngani wa kudhibiti biashara haramu ya mitandao maarufu kama upatu ambayo ina athari kubwa na wanawake wengi wameathirika nayo, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Ashatu Kijaji alisema biashara hiyo ni haramu.

Alisema hakuna taasisi yenye leseni ya kufanya biashara hiyo na kuwataka wananchi kutoa taarifa na kutojihusisha nazo kutafuta mitaji. Alisema ipo sheria kudhibiti taasisi za fedha zilizopewa kibali cha kuwasaidia wananchi, wanawake na vijana kupata mikopo bila riba. Alisema kanuni za sheria zimeshatengenezwa na zitaanza kutumika Julai mwaka huu na kuwataka wanawake na vijana kutumia fursa hiyo kupata mikopo ya fedha kwa biashara.

Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Dar es Salaam, Mhashamu ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi