loader
Picha

Wenye viwanja kuzunguka stendi Iringa kuhamishwa

MKUU wa Mkoa wa Iringa, Ally Hapi ametoa siku 30 kwa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa kuhakikisha stendi mpya ya mabasi yaendayo mikoani ya mjini Iringa inaanza kutumika.

Pia ameagiza wenye viwanja vinavyozunguka stendi hiyo kuondolewa na kupewa maeneo mengine. Awamu ya kwanza ya ujenzi wa stendi hiyo iliyopo Igumbilo, pembezoni mwa mji wa Iringa iliyogharimu zaidi ya Sh bilioni 3.7 ilikamilika mwaka mmoja na nusu uliopita, tangu wakati huo imekuwa haitumiki.

Mhandisi wa halmashauri hiyo, Richard Moshi akizungumzia hilo alisema: “Tulikuwa tunasubiri Sh bilioni 4.6 zingine kwa ajili ya ujenzi wa jengo la utawala na barabara zinazoingia na kuzunguka stendi hiyo kwa kiwango cha lami. Katika ziara yake iliyomfikisha katika stendi hiyo juzi, Mkuu wa Mkoa alionekana kushangazwa alipoelezewa sababu za stendi hiyo kutoanza kufanya kazi.

“Mimi sijaridhika kabisa, eti stendi hii haifanyi kazi kwa sababu haina barabara za lami, kwani kuna stendi ngapi kama hizi zimeanza kufanya kazi bila hizo barabara za lami,” alisema na kuuliza mapato ambayo halmasºhauri hiyo imepoteza kutokana na changamoto hiyo. Mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Hamid Njovu alisema wanakadiria kukusanya wastani wa Sh milioni 250 kwa mwezi endapo stendi hiyo itaanza kufanya kazi.

“Kwa hesabu hiyo mmepoteza wastani wa Sh bilioni 4.5 katika kipindi cha mwaka mmoja na nusu ambao stendi hiyo imekuwa haifanyi kazi,” alisema. Akizungumzia changamoto ya stendi hiyo kuzungukwa na viwanja vya watu, Mkuu wa Mkoa alisema kwa kuwa ardhi ni mali ya serikali, halmashauri hiyo inatakiwa kuwafutia umiliki wahusika kwa kuwapa viwanja vingine sehemu nyingine.

“Futeni hati zao na wapeni viwanja vingine, maeneo yanayozunguka stendi hiyo yawe mali ya serikali, tuweke hoteli, maduka, biashara zingine zinazoweza kuiingizia halmashauri mapato zaidi, stendi hii iwe moja ya vyanzo vikubwa vya mapato ya manispaa,” alisema.

Alisema stendi hiyo ni moja ya miradi ya kimkakati na kwamba ni lazima itumike kuongeza mapato ya halmashauri kwa kuzingatia kwamba kuna baadhi ya vyanzo vingine vya mapato vimechukuliwa na Serikali Kuu.

Wakati huohuo, Mkuu wa Mkoa ametembelea daraja la Igumbilo la mjini Iringa lililojengwa kwa zaidi ya Sh bilioni tano na kuishauri manispaa hiyo kujenga sehemu ya kupumzikia na ya michezo ya watoto kandokando ya daraja hilo lililojengwa katika mto Ruaha Mdogo. Mbali na kutembelea daraja hilo, alitembelea pia ujenzi wa soko la kisasa la ghorofa moja linalojengwa katika eneo la Mlandege mjini Iringa. Mkuu wa Mkoa alitoa siku 60 kwa Kampuni ya Home Africa Investment Corporation Ltd ya jijini Dar es Salaam inayojenga soko hilo kukamilisha ujenzi wake.

Awali ujenzi wa soko hilo utakaogharimu zaidi ya Sh bilioni 3.7 hadi kukamilika kwake; ulikuwa ukamilike Septemba, mwaka jana kabla mkandarasi huyo hajaongezewa miezi mingine sita hadi Juni, mwaka huu. “Nataka nitakaporudi hapa mapema Agosti, mradi huu wa soko uwe umekamilika. Vinginevyo serikali italazimika kuchukua hatua za kisheria dhidi ya mkandarasi,” alisema huku mhandisi wa manispaa hiyo akisema hadi sasa umekamilika kwa asilimia 80 tu. Aidha Hapi alishauri yafanyike maboresho katika soko hilo yatakayowezesha huduma nyingi zaidi kupatikana ikiwa ni pamoja na maduka makubwa, michezo ya watoto na sehemu za kufanyia mazoezi.

BENKI ya NMB imezindua 'NMB Afya loan', ...

foto
Mwandishi: Frank Leonard, Iringa

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi