loader
Picha

Serikali yapitia upya sheria ya leseni ndogo za madini

NAIBU Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo amesema wizara inapitia upya sheria ya utoaji wa leseni ndogo za biashara ya madini na wachimbaji, ambayo kwa sasa utekelezaji wake unazingatia kila kipindi cha kuanza kwa mwaka wa fedha wa serikali.

Alisema hayo hivi karibuni mjini Mahenge wilayani Ulanga, mkoa wa Morogoro baada ya kupokea malalamiko ya wafanyabiashara wa madini wa wilaya hiyo wakati wa uzinduzi wa soko la madini la Mahenge. Alisema sheria za leseni za uchimbaji madini zinaanza kutolewa kila Julai mosi na kumalizika Juni 30, mwisho mwa mwaka wa fedha wa serikali.

Alisema jambo hilo limelalamikiwa na waombaji wa leseni ndogo za biashara ya madini na wachimbaji wakiwemo wa migodi ya Mahenge. “Wizara tumeliona na tunaifanyia marekebisho sheria ili leseni iweze kukatwa wakati wowote bila kuangalia ni mwezi gani,” alisema. Mabadiliko ya sheria hiyo inakusudia kumwezesha mchimbaji wa madini na mfanyabiashara kukata leseni mwezi wowote bila kufuata kalenda ya mwaka wa fedha wa serikali.

“Mfano mtu akikata leseni Agosti mosi, mwaka huu atahesabiwa kipindi chake cha mwaka mmoja hadi Julai 30, 2020 na hapo atalazimika kulipia tena leseni yake kwa mwaka mwingine,” alisema. Kwa upande wa masoko ya madini, Naibu Waziri alisema kuwa serikali haitarajii kuona kunajitokeza ukiritimba na vikwazo kwa wauzaji na wanunuzi katika masoko yanayofunguliwa mikoa mbalimbali nchini.

“Tumeibiwa sana kupitia mikataba mibovu, sasa mimi na waziri wangu pamoja na wizara tumesema tutahakikisha tunalala mbele na watoroshaji mpaka kieleweke,” alisema Nyongo na kuongeza: “Tunataka fedha kutoka sekta ya madini, hatumchekei mtu na wala hatubabaishani na mtu, ndiyo maana tumeweka masoko haya ili wachimbaji wanufaike na serikali ipate kodi yake “.

Naye Mwenyekiti wa Wachimbaji Madini Wilaya ya Ulanga, Protas Lunkombe alisema sheria ya sasa inamtaka mchimbaji kukata leseni kila mwanzo wa mwaka wa fedha wa serikali. Badala yake sheria hiyo ifanyiwe marekebisho ili kuwezesha leseni ziwe zinakatwa mwezi wowote ili kuwawezesha wenye mitaji wanaohitaji kuingia katika uchimbaji wa madini wasisite kutokana kwa kubanwa na sheria.

Mkuu wa wilaya ya Ulanga, Ngollo Malenya alisema licha ya wilaya ya Ulanga kuwa na utajiri mkubwa wa madini, lakini wachimbaji wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikuwemo ukosefu wa elimu ya kutosha juu ya sekta nzima ya madini . Malenya pia alisema leseni nyingi za wamiliki wadogo hazifanyi kazi, hivyo kuzuia uhalali kwa wenye uhitaji kupata leseni za kuendelea na uchimbaji wa madini.

Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Dar es Salaam, Mhashamu ...

foto
Mwandishi: Stanslaus Nyongo

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi