loader
Picha

…Kutumia jezi mpya, Makonda aonya

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amezindua jezi mpya ambazo zitatumiwa na timu ya soka ya Taifa, Taifa Stars katika Mashindano ya Mataifa ya Afrika (Afcon 2019).

Akizundua jezi hizo Dar es Salaam jana, Makonda aliwaonya wale wenye tabia ya kutengeneza jezi feki za Taifa Stars na kuziuza, kuwa watachukuliwa hatua kali za kisheria. Haflaya uzinduzi huo iliyofanyika kwenye Hoteli ya Serena na kuhudhuriwa na watu mbalimbali, wakiwemo viongozi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).

Makonda alisema kuna watu wana tabia ya kutengeneza jezi feki na kuziuza kiholela, hivyo wasijaribu kufanya hivyo katika jezi za Taifa Stars, kwani watachukulia hatua kali. Jezi za nyumbani za Taifa Stars zina rangi ya bluu wakati zile za ugenini zina rangi ya njano, huku zikiwa na picha ya twiga sehemu ya chini ya jezi hiyo upande wa kulia. Makonda alisema kuwa makampuni 40 kati ya 100 yameichangia Stars Sh milioni 400 baada ya kila moja kutoa kiasi cha Sh milioni 10 na kuyaomba makampuni mengine kujitokeza kuendelea kuichangia timu hiyo.

Mkuu huyo wa mkoa ambaye ni mjumbe wa Kamati ya Kusaidia Stars ishinde alipewa jezi 100 kwa ajili ya kuwagawia wajumbe wa kamati hiyo pamoja na watu wengine. Aidha, Stars ambayo tayari iko Misri ikijiandaa na Mashindano ya Mataifa ya Afrika na leo itajipima nguvu dhidi ya wenyeji Misri, kwa mara ya kwanza itavaa jezi za ugenini, ambazo watatumia katika mashindano hayo ya Afcon 2019.

Rais wa TFF, Wallace Karia alisema kuwa jezi hizo ndizo rasmi za Taifa Stars na zitatumika kwa timu zote za taifa kuanzia ile ya wakubwa, vijana na ile ya wanawake (Twiga Stars). Alisema jezi hizo zitauzwa katika maduka maalumu na zitasaidia kuongeza mapato ya Serikali.

Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Dar es Salaam, Mhashamu ...

foto
Mwandishi: Tuzo Mapunda

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi