loader
Picha

Kocha mpya Azam kuangalia vijana

KOCHA Mkuu wa Azam FC, Ettiene Ndayiragije amesema ataendelea kusimamia falsafa ya vijana kwenye timu yake mpya kuiwezesha klabu hiyo kufi kia malengo yaliyokusudiwa.

Ndayiragije aliyesaini mkataba wa miaka miwili jana na kutambulishwa kwa waandishi wa habari, alisema elimu ya ukocha ya kiwango cha juu aliyonayo inampa nafasi ya kuchagua vijana bora.

Alisema kwa elimu yake anaweza kuwa kocha wa viungo, wa makipa na bado akachambua vijana na kwamba wakiaminiwa wanaweza hata kupambana kwenye michuano ya kimataifa.

“Nimefanya kozi mbalimbali za ukocha wa kiwango cha juu, najua kufundisha, kuteua vijana mipango yangu ni kuendeleza falsafa ya vijana,” alisema na kuongeza kuwa atawatizama baadhi ya vijana kutoka kituo cha michezo cha Azam na kuwapandisha.

Kocha huyo mwenye uzoefu na soka la hapa nchini inakuwa ni timu yake ya tatu kwa Tanzania baada ya kufanya vizuri akiwa Mbao FC na KMC kwa vipindi tofauti ambako nako alitumia falsafa ya vijana na baadhi ya wakongwe.

WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na ...

foto
Mwandishi: Grace Mkojera

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi