loader
Picha

Peter Isare Kijana aliyekataa kujibweteka na kujiajiri

VIJANA wanaomaliza elimu ya juu wanatakiwa kuachana na fikra za kutaka kuajiriwa na serikali na badala yake wafikirie kutumia elimu yao kwa lengo la kubuni miradi mbalimbali ambayo itawawezesha kujiajiri wenyewe.

“Kiukweli siamini katika kuajiriwa, napenda kujiajiri na kutoa fursa za ajira kwa vijana wenzangu ambao wamekosa fursa hiyo na huku wakiwa na sifa,” anasema Peter Isare, muasisi na mkurugenzi wa Kampuni ya Jenga Afya, Tokomeza Umaskini (JATU).

Anasema tangu alipomaliza chuo Kam Kkikuu hakuwa na wazo la kuajiriwa na wazo lake kuu ilikuwa kufanya kitu ambacho kitamuwezesha kujiajiri mwenyewe. Isare (29) ni mhitimu wa Shahada ya Sheria kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) ambaye ameamua kujikita katika kilimo, viwanda na masoko ili aweze kujikwamua kiuchumi, kwani aliamini katika kilimo cha mazao ya chakula kwa sababu ni bidhaa inayoweza kutumiwa na watu wote.

Anasema licha ya kuwa tayari na wazo la kuanzisha biashara hiyo baada ya kuona fursa za masoko zilizopo hakuwa na mtaji wa kufanikisha ndoto hizo. “Ilikuwa 2016 nilimshirikisha wazo langu rafiki yangu anayeitwa Issa Simbano ambaye alilipokea wazo langu na baada ya kumaliza chuo mwezi Julai mwaka 2016 nikaanza mchakato wa kusaka fedha za kusajili kampuni na mwaka huo huo mwezi Oktoba kabla ya sherehe za kumaliza chuo nikawa nimefanikiwa kusajili kampuni yetu Brela na tuliandaa mpango kazi wetu ambao ulianza rasmi Januari 2017… lakini nikasema ili tuweze kufanikiwa dhamira yetu ni lazima tuwe na kikosi kazi, basi tukashirikisha watu wengine ambao tulimaliza nao chuo ambao tuliamini tutaweza kufanya nao kazi maana sisi ni wanasheria, ndio tukachukua mtu wa IT, tukachukua mtu wa masoko, tukachukua wataalamu wa kilimo tukawa na timu yetu,” anasema.

Hata hivyo, Isare anasema hawakuwa na fedha na wakaanza kushikana mashati, wakiamua kila mtu afanye anavyojua kupata fedha za mtaji wa kuanzisha mpango hu. “Tukasema ni boom lako limebaki, kama utaiba, utakaba lakini ipatikane si chini ya milioni tatu, basi wakati tunapambana, tukafanikiwa kupata Sh 3,600, 000 … lakini pia mwaka huo huo wa 2016 benki ya DCB walianzisha mikopo kwa vijana, tukajikusanya tukaunda kikundi, tukaenda kuchukua mkopo ndio tukaanza kusaga unga na kuongezea thamani na kuanza kuuza.

Wakati tunaanza vifungashio tulikuwa tunaandika kwa ‘marker pen’ lakini jamii tunashukuru ilitukubali, wakawa wanatuunga mkono bidhaa zetu, tukaanza hivyo mpaka sasa tumekuwa,”anasema Isare. Anasema pia waliweza kutanua biashara yao baada ya ofisi ya Waziri Mkuu chini ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi , Ajira, Vijana na Walemavu, Jenista Mhagama baada ya kutangaza shindano la andiko kwa vijana ambao wao walikuwa miongoni mwa vijana 10 ambao waliwasilisha wazo lao likapita na kupatiwa mkopo wa Sh milioni 10, mkopo uliowawezesha kutanua biashara yao kwa kununua mashamba Kiteto, Kilombero na Tanga.

“Mwaka 2016 ofisi ya waziri mkuu ilianzisha vijana wabunifu tukapeleka wazo letu la Jatu tukashinda, tukaenda Simiyu kwenye maonesho, kupitia wao tumejifunza na kupanua wigo mkubwa,”anasema. Kwa mujibu wa Isare kampuni hiyo waliisajili kuwa ya umma na mpaka sasa wamefanikiwa katika kilimo cha mpunga Kilombero, Man- yara kilimo cha alizeti na mahindi na Tanga kilimo cha maharage na kuwa wanawawezesha wakulima kulima kilimo cha kisasa na kuwapatia wataalamu ambao wanawapa elimu ya kufanya kilimo cha muda wote kisichotegemea hali ya hewa.

“Igima tuna kiwanda cha kukoboa mchele, Kibaigwa kiwanda cha mahindi na alizeti, tunaunganisha kilimo na viwanda na soko tumelitengeneza wenyewe. Jatu unaponunua chochote kama chakula ni rahisi kukuza faida tuna mfumo rasmi wa kugawa faida, mteja ambaye ni mwanachama akinunua bidhaa anapata bonasi ambapo gawio analipata mwisho wa mwezi.

Kilimo kinalipa ukikitilia maanani, Jatu tuna watu zaidi ya 13,000 ambao wanafanya kilimo na biashara,”anasema. Isare anafafanua kuwa unaweza kujiunga kwa kuuza bidhaa ukapata mgawo kila mwezi au ujiunge kwenye kilimo au kununua hisa kupata gawiwo ukapata faida kutokana na faida ya kampuni. Kuingia soko la Hisa Anasema wapo kwenye mchakato wa kuingia katika soko la hisa (DSE) ifikapo mwezi Agosti kwa mtaji wa Sh bilioni 7.5 na kutaka watanzania kuchangamkia hisa hizo ili kujikomboa kiuchumi.

Isare anasema mpango kazi wao wanatarajia ifikapo mwaka 2022, wawe wamefanikiwa zaidi kwenye kilimo kwa kuwa kwa sasa wanalima kilimo cha kawaida ambapo hakizidi ekari 5,000 na kwamba hadi ifikapo mwaka huo watakuwa na zana za uhakika, kufanya kilimo cha umwagiliaji, kama ilikuwa wanalima ekari moja basi ni kulima ekari 10 hadi 15 na kwamba watawekeza mitambo ya umwagiliaji na kutengeneza miundombinu.

“Shambani hapo hapo kutakuwa na huduma za kijamii ikiwemo kuweka kiwanda, kitakachoongezea bidhaa zetu ubora, tunahitaji kuboresha viwanda vyetu viwe vingi na vya kisasa, kuzalisha kwa kiwango cha juu kwa ubora wa juu zaidi,” anasema.

Isare anasema watu wengi wanapata changamoto kwenye masuala mbalimbali kutokana na umasikini wanashindwa kumudu gharama za maisha na kusababisha migogoro kwenye jamii Kijana huyo ambaye ni mwenyeji wa Mara anasema kabla ya Jatu PLC, mwaka 2015 alisajili shirika lisilokuwa la kiserikali lililojulikana kama Legal Protection and Life Improvement Organization, likiwa na lengo la kutetea haki za binadamu hususani wanawake.

NGOs hii ipo kwa ajili ya kutetea haki za binadamu, ya msingi kila mtu anaheshimiwe kwa nafasi yake na habugudhiwi kwa kuwa anaweza kujiongoza yeye mwenyewe, unyanyasaji na vitu vyote hivyo vinapigwa vita. “Historia ya Mara wanawake hawamiliki kipato, wanaume wamebeba jukumu la kumiliki kila kitu, hivyo wanawake wanakuwa hawana sauti, ili uwe na sauti lazima uwe na kipato, ndio kupitia NGOs hii na kukithiri kwa matukio ya ukatili mkoani Mara ikatusukuma kuanzisha Jatu ili pia tuwasaidie kwa kuwainua kiuchumi,” anasema.

Peter Isare (29) ni mtoto wa pili kati ya watoto saba, mzaliwa wa Mkoa wa Mara, alisoma shule ya msingi Kenyamusabi iliyopo Tarime Vijijini na kumaliza elimu yake ya msingi mwaka 2005.

Mwaka 2006 alijiunga na shule ya sekondari Nyanungu ambapo baadaye alihamia shule ya Mshikamano iliyopo Musoma Mjini na kuhitimu kidato cha nne mwaka 2009 na kufaulu vizuri. Mwaka 2010 alijiunga kidato cha tano na sita katika shule ya vipaji maalum ya Ilboru na kuhitimu mwaka 2012 na kuchaguliwa kujiunga Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kuchukua ambapo alihitimu Shahada ya Sheria.

“Dhamira yangu siku zote ni kufanya kazi kwa bidii na ...

foto
Mwandishi: Vicky Kimaro

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi