loader
Picha

Sheria 1 kusimamia uwekezaji

SERIKALI inajiandaa kuwasilisha bungeni muswada wa sheria kuhusu uwekezaji ili kuwe na sheria moja inayosimamia uwekezaji kwa lengo la kuweka mazingira rafiki ya kufanya biashara.

Waziri wa Nchi katika Ofi si ya Waziri Mkuu (Uwekezaji), Angellah Kairuki amesema hayo jijini Dar es Salaam wakati anafungua kongamano la wafanyabiashara wanawake lililoandaliwa na Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) lenye lengo la kusikiliza kero za wafanyabiashara wanawake nchini.

Amesema, sheria itakayotungwa itapunguza utitiri wa vikwazo vinavyotokana na kutokuwa na mfumo rafiki kwenye uwekezaji.

Waziri Kairuki ameyasema, hayo baada ya kusikiliza baadhi ya kero za wafanyabiashara wanawake.

Aidha aliwataka wajenge umoja, wajiamini na kufanya kazi kwa bidii ili kuinua vipato vyao pamoja na kujenga uchumi wa nchi.

Akielezea dhumuni la kuwakutanisha wafanyabiashara hao, Mwakilishi wa Wanawake Wazalishaji wa Bodi ya TPSF, Fatma Abdallah alisema taasisi hiyo imewakutanisha wanawake ili kuibua fursa mbalimbali za kiuwekezaji, lakini pia kujadili changamoto wanazozipata.

Rais wa Sauti ya Wanawake Wajasiriamali Tanzania (VOWET), Maida Waziri alisema kuwa kuna changamoto kubwa kwa wajasiriamali wanawake hasa kwenye urasimishaji wa biashara zao, lakini ni vyema serikali ikaangalia zaidi sera na sheria zilizo rafiki ili kupunguza hatari ya kuwakatisha tamaa wafanyabiashara.

Maida pia aliiomba Serikali kuangalia uwezekano wa kutoa fursa kwa wajasiriamali kwenye vyuo mbalimbali ili waweze kuelimishwa juu ya mazingira na jinsi ya kuwekeza.

“Kuna changamoto ya elimu, lakini TPSF na Taasisi ya Biashara, Viwanda na Kilimo (TCCIA) ina jukumu la kutoa mafunzo lakini pia serikali kupitia vyuo mbalimbali vya ufundi na biashara vinaweza kutoa msaada wa bure kwa wafanyabiashara wenye lengo la kuwainua,” alisema Rais huyo.

Kwa upande wa Mwakilishi wa Chama cha Wachonga Vinyago cha Tanzania (TANCRAFT), Louise Mushi alieleza kuwa, wajasiriamali wengi wanawake wanakabiliwa na miundombinu ya kufanyia kazi sambamba na mazingira bora ya kufanya biashara kwenye maeneo ya mipaka.

Mwakilishi wa Chama cha Wanawake Wachimbaji Madini Tanzania (TAWOMA), Leilla Jumbe alisema kuwa changamoto kubwa inayowakabili wanawake wengi ni mitaji na kwamba inatokana na wanawake wange kutokuwa na mali au ardhi kwa ajili ya kuweka dhamana.

Mkoa wa Pwani umebaini kuwa maonesho ya bidhaa zinazozalishwa viwandani ...

foto
Mwandishi: Alfred Lasteck

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi