loader
Picha

Mechi zote AFCON kwa lugha ya Kiswahili- DSTV

KAMPUNI ya MultiChoice Tanzania imejipanga kuonesha michezo yote ya michuano ya Afcon 2019 itakayoanza kesho kutwa nchini Misri kwa lugha ya Kiswahili.

Akizungumza mapema leo na wanahabari wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN), Ofisa Masoko wa MultiChoice, Shumbana Walwa alisema matangazo ya michezo yote ya michuano hiyo yatakuja mubashara kwa lugha ya Kiswahili.

“Tutarusha mechi zote 52 ya michuano hiyo kwa lugha ya Kiswahili na watanzania wote wenye vingamuzi vya DSTV wataweza kushuhudia mechi hizo zikitangazwa na lugha adhimu chini ya wachambuzi makini,” alisema ofisa huyo.

Ofisa huyo alitaja baadhi ya wachambuzi wa michezo nchini watakaofanya shughuli hiyo kuwa ni Salama Jabir, Edo Kumwembe, Ibrahim Masoud, Oscar Oscar, Aboubakar Liongo na Maulid Kitenge.

Akizungumza kwa niaba ya wachambuzi wengine watakaoshiriki kurusha matangazo kwa lugha ya Kiswahili, Salama Jabir alisema kwa mara ya kwanza watatangaza michezo ya AFCON kwa Kiswahili.

“Naamini kila kitu kinawezekana kwani kwenye nia pana njia na mimi pamoja na wezangu tutahakikisha kuwa tutawapa kilicho bora na kinachovutia,”alisema.

MSHAMBULIAJI wa Kimataifa wa Simba, raia wa Burundi, Meddie Kagere ...

foto
Mwandishi: Rahimu Fadhili

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi