loader
Picha

Wafanyabiashara wakubwa wabanwa madeni sugu

WIZARA ya Fedha na Mipango imetoa orodha ya kwanza ya wadaiwa sugu wafanyabiashara 15 walionufaika na Mpango wa Kusaidia Uingizwaji wa Bidhaa nchini (CIS) na FACF, wafanyabiashara Mohamed Dewji na Yusuf Manji ni kati ya wadaiwa hao.

Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa jana na wizara hiyo, imewataka wadaiwa hao kulipa madeni yao haraka iwezekanavyo kabla hatua za kisheria kuchukuliwa. Watu wengine mashuhuri waliopo kwenye orodha hiyo ni pamoja na mwanasiasa aliyekuwa Waziri kwenye utawala uliopita, Stephen Wassira kupitia kampuni yake ya Siza Cold Storage Co. Ltd pia mwanasiasa Hashim Rungwe kupitia kampuni yake ya Bahari Motor Co. Ltd.

Ikizungumzia madeni hayo, taarifa hiyo ilifafanua kuwa yanatokana na mkopo wa masharti nafuu kwa Taasisi, Kampuni, Viwanda na Wafanyabiashara ambapo wakopaji walitakiwa kulipa deni husika bila ya kutozwa riba katika kipindi cha miezi 18 tangu muda waliopewa mikopo hiyo.

Ilinukuu kifungu cha sheria cha CIS ya mwaka 2008 (1)(b), inayosema kuwa mkopaji akichelewa kulipa katika kipindi cha miezi 18 tangu kupatiwa mkopo, atapaswa kulipa riba ya asilimia sawa na kiwango kinachotozwa na Benki Kuu ya Tanzania (BoT) inapoikopesha serikali katika kipindi husika. Ilielezea kuwa zaidi ya kampuni 980 zimekopeshwa chini ya utaratibu huo ambapo tangazo hilo lililotolewa jana lilikuwa ni la mara ya mwisho kwa kuwa imeshatangaza mara kwa mara na wadaiwa wameshindwa kuitikia mwito.

Ilisema matangazo yalitolewa mnamo Desemba 30 mwaka 2015 na Aprili 4 mwaka jana, lakini hakuna jitihada za ulipaji wa madeni hayo zilizofanyika. Ilielezea kuwa wadaiwa ambao majina yao yametajwa jana kwa hiyo mara ya mwisho wakishindwa kujitokeza na kulipa hatua za kisheria zitachukuliwa. Kwa upande wa mfanyabiashara Mohamed Dewji anadaiwa kupitia kampuni zake za 21st Century Textiles na Afritex Ltd huku Manji akidaiwa kupitia kampuni zake za Farm Equipment Tanzania Ltd, Quality Group Ltd, Dunhill Motors Ltd, Quality Seed Ltd, Quality Garage Ltd.

Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kwa kushirikiana na Taasisi ya ...

foto
Mwandishi: Evance Ng’ingo

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi