loader
Picha

Wabunge waipa mwongozo TRA

MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) inaweza kukusanya Sh trilioni 1.7 kwa mwezi endapo itaongeza vyanzo vipya vya kodi, itadhibiti wanaoharibu mashine za kielektroniki (EDF) na itaipa kipaumbele sekta binafsi ambayo ni injini ya uchumi wa nchi.

Akichangia bajeti ya Fedha na Mpango, Mbunge wa Muleba Kaskazini, Charles Mwijage alisema TRA itafanikiwa kukusanya Sh trilioni 1.7 kutoka Sh trilioni 1.3 za sasa kama itatekeleza mpango wa kuboresha biashara (blue print) kwa kuipa fursa ya kutosha sekta binafsi katika kuendesha uchumi.

Alisema mpango huo (blue print) unatakiwa kusimamiwa na Rais John Magufuli kwa kuitisha mikutano na viongozi wa serikali na sekta binafsi ili kujadiliana namna ya kuufikia uchumi wa kati na misafara ya kwenda Ikulu kwa makundi mbalimbali wafanyabiashara, wachimbaji madini na wengine itamalizika.

Alisema mpango huo unatakiwa kusimamiwa na Rais Mafuguli kama ambavyo India umesimamiwa na Waziri Mkuu wa India, Narendra Modi na nchini Rwanda unasimamiwa na Rais Paul Kagame na umefanikiwa nchi hizo kusonga mbele kiuchumi. Mwijage alisema mpango huo unaonesha wazi kwamba sekta binafsi ndiyo inayoendesha biashara nchini, hivyo katika kutekeleza mpango huo, serikali inatakiwa kuipa msukumo sekta hiyo ili kutoa mchango mkubwa katika kufikia uchumi wa kati 2025.

Mwijage alisema TRA itaweza kufikia makusanyo hayo kama sekta binafsi itapewa msukumo ili kuwa imara na yenye ushindani kwa kushawishi wafanyabiashara wengi kulipa kodi kwani ndio wanaosimamia sekta mbalimbali nchini zikiwemo za kilimo, uvuvi, mifugo, usafiri na usafirishaji na nyingine.

Mbunge wa Tarime Mjini, Esta Matiko (Chadema) alisema TRA itaweza kuongeza makusanyo kama itaongeza vyanzo vya mapato hasa kuimarisha matumizi ya ufukwe wa bahari kuu kutoka Tanga hadi Mtwara ambao haujatumika vizuri hadi sasa.

Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kwa kushirikiana na Taasisi ya ...

foto
Mwandishi: Magnus Mahenge, Dodoma

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi