loader
Picha

Dola 500 zapatikana kuboresha huduma za maji

SERIKALI imepata dola za Marekani milioni 500 kwa ajili ya kuboresha huduma za maji katika miji 28 nchini na ujenzi wa miradi hiyo utaanza mwaka huu wa fedha wa 2019/20.

Naibu Waziri wa Maji, Jumaa Aweso, aliliambia Bunge jana wakati akijibu swali la msingi la Mbunge wa Kilombero, Peter Lijualikali (Chadema), aliyehoji serikali ina mpango gani wa kuongeza mtandao wa maji katika mji wa Ifakara.

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri alisema mji mdogo wa Ifakara una wakazi 122,688 na hali ya upatikanaji wa maji katika mji huo ni asilimia 35 na kwamba mahitaji ni mita za ujazo 7,008 lakini yanayopatikana kwa sasa ni lita za ujazo 1,004.

“Mji huo wa Ifakara unapata maji wastani wa asilimia 35, serikali ina mpango wa muda mrefu na mfupi wa kuhakikisha mji huo na mingine inapata maji ya kutosha na ndio maana tumepata fedha kutoka serikali ya India Dola za Marekani milioni 500 kwa ajili ya kuboresha huduma za maji kwenye miji 28 ya Tanzania Bara na Zanzibar na Ifakara itafaidika pia,” alisema Aweso.

Aidha, alisema katika mpango wa muda mfupi serikali kupitia Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mogorogo, imekamilisha mradi wa uboreshaji wa huduma ya maji katika mji huo.

Aweso alisema kazi zilizokamilika katika mpango huo ni ujenzi wa nyumba za pampu, ufungaji wa pampu mbili na ujenzi wa mtandao wa bomba la kilomita 8.4 Alisema katika mpango huo wa muda mrefu ambao pesa hiyo dola milioni 500 zimepatikana hivi sasa serikali inaandaa utaratibu wa kuwapata wataalamu washauri watakaofanya usanifu wa kina na kuandaa makabrasha ya zabuni.

Aweso alisema kukamilika kwa mipango hiyo ya muda mrefu na mfupi kutaboresha hali ya upatikanaji wa maji katika mji wa Ifakara na kufikia asilimia 90 ya upatikanaji wa maji ifikapo mwakani.

NAIBU Waziri wa Maliasili na Utalii, Constantine Kanyasu ametoa maagizo ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi