loader
Picha

Brela yarahisisha usajili wa biashara

WAKALA wa Usajili wa Kampuni na Leseni za Biashara (Brela) imerahisisha utaratibu kwa wananchi kusajili biashara zao kutoka mfumo wa kawaida kwenda wa kidijiti, jambo litakalorahisisha usajili kwa muda mfupi.

Mkurugenzi wa Huduma za Biashara na Fedha wa Brela, Bakali Mketo alisema jana akifungua semina ya siku tatu ya maofisa biashara na wadau ukumbi wa Katibu Tawala mkoa Arusha.

Alisema wanataka kuhakikisha huduma hizo ziko karibu na wananchi na wanatumia maofisa biashara wa halmashauri kuhamasisha wananchi kutumia mitandao kujisajili kuondoa usumbufu. Alisema Brela inatoa elimu kwa umma ili kuelewa umuhimu wa kusajili biashara na majina ya kampuni zao ili kuwawezesha kufanya biashara mbalimbali wakiwa na utambulisho wa bidhaa zao kwenye masoko.

Alisema kujisajili kwa mtandao kutamwezesha mlengwa kufanya biashara inayotambulika na hivyo kuingia kwenye mfumo wa ushindani kwenye masoko mbalimbali nchini na nje pia. Mketo alisema kusajili bidhaa kupitia Brela, kunamwezesha mfanyabiashara nchini kuwa na hati miliki ya jina lake la bidhaa ambalo haliwezi kutumiwa na mtu mwingine kibiashara.

“ Tangu tumetambulisha mfumo mpya wa usajili, kampuni 7,000 zimesajiliwa. Tulianza kusajili kampuni 60 kwa mwezi lakini hadi sasa tunasajili 750 hadi 800 kwa mwezi,” alisema.

Ofisa Biashara Halmashauri ya Jiji la Arusha, Vitus Athanas, alisema changamoto Brela ni kutokuwa na ofisi za kutosha na hivyo kuwepo usumbufu kwa baadhi ya wafanyabiashara ambao hulazimika kwenda kwa wanasheria ili kusajili biashara zao na kuongezea gharama. Alisema semina hizo zitasaidia kuwapatia wafanyabiashara uelewa wa umuhimu wa kusajili biashara zao ambapo pia wataweza kuwa na majina ya bidhaa zao kwenye masoko.

NAIBU Waziri wa Maliasili na Utalii, Constantine Kanyasu ametoa maagizo ...

foto
Mwandishi: John Mhala, Arusha

1 Comments

  • avatar
    Seba
    06/09/2019

    Toeni app tunayoweza kuipakua kupitia PLAYSTORE

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi