loader
Picha

Idadi ya watu duniani kufikia bil 9.7

IDADI ya watu duniani inatarajiwa kuongezeka na kufi kia bilioni 9.7 mwaka 2050 kutoka bilioni 7.7 ya sasa, ambapo barani Afrika inatarajiwa kuongezeka mara mbili.

Ripoti ya idadi ya watu duniani ya Idara ya Mambo ya Kiuchumi na Kijamii ya Umoja wa Mataifa ilisema idadi ya watu inatarajiwa kufikia bilioni 11 mwaka 2100. Idadi ya watu katika nchi kadhaa zinazoendelea imeongezeka kutokana na ongezeko la matarajio ya maisha, wakati kiwango cha ukuaji wa dunia kimeshuka kwa sababu ya kushuka kwa viwango ya uzazi.

Ripoti hiyo ilisema kufikia mwaka 2050, zaidi ya nusu ya ukuaji wa idadi ya watu duniani utaelekezwa katika nchi tisa. Nchi hizo ni India, Nigeria, Pakistan, Jamhuri ya Kimokrasi ya Congo(DRC), Ethiopia, Tanzania, Indonesia, Misri na Marekani.

China yenye idadi kubwa zaidi ya watu duniani itashuhudia idadi ya watu wake ikipungua kwa silimia 2.2 au kati ya mwaka 2019 na 2050. Nchi 27 zimekuwa na upungufu wa asilimia moja ya idadi ya watu tangu mwaka 2010 kutokana na viwango vya chini ya uzazi.

Ripoti hiyo ya Umoja wa Mataifa ilisema vifo sasa vinazidi vizazi vipya katika mataifa ya Belarus, Estonia, Ujerumani, Hungary, Italia, Japan, Urusi, Serbia na Ukraine. Viwango vya jumla vya uzazi duniani ambavyo vilishuka kutoka vizazi 3.2 kwa mwanamke mwaka 1990 hadi 2.5 mwaka huu vinatarajiwa kushuka zaidi hadi 2.2 mwaka 2050.

Pia ripoti hiyo inakadiria matarajio ya jumla ya maisha, ikiwemo katika nchi maskini ambako sasa ni miaka saba chini zaidi ya wastani wa duniani. Kwa mujibu wa ripoti wastani wa dunia wa matarajio ya maisha unapaswa kufikia miaka 77.1 mwaka 2050 kutoka miaka 72.6 ya sasa. Mwaka 1990 wastani wa matarajio ya kuishi duniani ulikuwa miaka 64.2.

Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kwa kushirikiana na Taasisi ya ...

foto
Mwandishi: NEW YORK, Marekani

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi