loader
Picha

Mwalimu Mkuu atuhumiwa kumpa mimba mwanafunzi

MWALIMU Mkuu wa Shule ya Msingi Nyantore iliyopo Kijiji cha Kagongo Halmashauri ya wilaya Kigoma, Jackson Rwekaza anatuhumiwa kumpa ujauzito mwanafunzi wa darasa la saba katika shule hiyo na hivyo kusababisha kukatisha masomo ya mwanafunzi huyo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma, Pendo Mangali, alikiri ofisi yake kuwa na taarifa juu ya suala hilo na kwamba hatua za kiutumishi zimeanza kuchukuliwa.

Mangali alisema kuwa kupitia Tume ya Utumishi ya Walimu (TSD) wameanza kufanyia kazi suala hilo ikiwemo kuchunguza ukweli wa tuhuma hizo na ikithibitika hatua za kinidhamu na kiutumishi zitachukuliwa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, Martin Otieno, alisema mtuhumiwa alikamatwa na kuhojiwa kuhusiana na tuhuma zinazomkabili. Hata hivyo, Kamanda Ottieno alisema kuwa baada ya mahojiano mtuhumiwa aliachiwa kwa dhamana huku uchunguzi ukiendelea ili kubaini ukweli wa tuhumu dhidi yake.

Akizungumzia mkasa huo mwanafunzi huyo mwenye umri wa miaka 16, amekiri kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwalimu wake na kwamba amekuwa akija naye mjini Kigoma na kumnunulia vitu mbalimbali.

Mama mzazi wa mtoto huyo, Sakina Kazili ameeleza kusikitishwa na kitendo hicho na kuomba serikali kumchukulia hatua kali mtuhumiwa aliyetajwa kwa jina la Jackson Rwekaza ili haki iweze kutendeka inavyostahili.

Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kwa kushirikiana na Taasisi ya ...

foto
Mwandishi: Fadhili Abdallah, Kigoma

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi