loader
Picha

Mwantika kuimarisha beki Taifa Stars

BEKI mahiri nchini, David Mwantika amerudishwa katika kikosi cha Taifa Stars kilichopo Misri, kujiandaa na mashindano ya Mataifa ya Afrika (Afcon 2019) kuchukua nafasi ya Aggrey Moris aliyeumia nchini humo.

Morris aliumia wakati Taifa Stars ikicheza dhidi ya wenyeji Misri katika mchezo wa kimataifa wa kujipima nguvu, ambapo Stars ilifungwa bao 1-0 katika mchezo huo.

Mwantika alikuwepo katika kikosi cha awali cha timu hiyo, lakini alichujwa katika kikosi cha mwisho kabla ya kuanza kwa mechi za kirafiki.

Taifa Stars pia ilicheza na Zimbabwe katika mchezo mwingine wa kirafiki, ambao timu hizo zilitoka sare ya 1-1.

Michuano hiyo inatarajiwa kuanza kesho Juni 21 nchini humo, ambapo Taifa Stars iko katika Kundi C pamoja na Senegal, Algeria na Kenya. Bingwa mtetezi wa mashindano hayo ni Cameroon, ambayo imepania kutetea taji lao katika fainali hizo za 32 za Mataifa ya Afrika.

Msemaji wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Clifford Ndimbo amesema hajapata taarifa rasmi za kuitwa kwa mchezaji huyo na kama ni kweli hajui atakwenda Misri lini.

Wakati huohuo, timu ya taifa ya Ghana imeweka hadharani namba za jezi za kikosi chao, ambacho kitashiriki fainali hizo za Mataifa ya Afrika nchini Misri.

Nahodha wao Andre Ayew, Asamoah Gyan, Mubarak Wakaso na Thomas Partey wanaendelea kutumia namba za jezi zao walizotumia katika mashindano yaliyopita nchini Gabon.

Baba Rahman yeye atavaa jezi namba 17, Christian Atsu namba saba, Jordan Ayew amepewa jezi namba tisa na Afriyie Acquah yeye atatinga jezi namba sita. Wachezaji wageni katika timu hiyo, Thomas Agyapong, Kassim Nuhu, Joseph Aidoo wenyewe watavaa jezi namba tatu, 15 na 18.

Wachezaji wengine ambao wanaichezea timu hiyo kwa mara ya kwanza katika mashindano hayo ya Afcon 2019 ni Felix Annan atakayevaa jezi namba 16, wakati Lawrence Ati Zi Gi atatinga jezi namba 12.

TIMU za Ligi Kuu Tanzania Bara zimegomea mfumo mpya unaotarajiwa ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi