loader
Picha

DSTV kuonesha mechi zote Afcon 2019

KAMPUNI ya MultiChoice imetangaza kuonesha michezo yote ya michuano ya Afcon 2019 itakayoanza kesho nchini Misri.

Akizungumza katika chumba cha habari cha HabariLeo, mwakilishi wa DSTV, Shumbana Walwa amesema matangazo ya michuano hiyo yatakuja mubashara kwa lugha ya Kiswahili katika michezo yote 52 ya michuano hiyo.

Amesema mechi hizo zitarushwa na baadhi ya wadau na wachambuzi wa michezo nchini, akiwemo Salama Jabir, Edo Kumwembe, Ibrahim Masoud na wengineo.

Taifa Stars itacheza mchezo wa ufunguzi Jumapili dhidi ya Senegal na itacheza mchezo wa pili dhidi ya Algeria na kumaliza na majirani zao timu ya Taifa ya Kenya, Harambee Stars.

Wakati joto likiwa linapanda huku ikiwa imebaki siku moja kabla ya michuano ya AFCON kuanza, baadhi ya timu tayari zimekamilisha maandalizi yake kwa ajili ya kuhakikisha zinafanya vizuri katika michuano hiyo.

Timu ya Taifa, Taifa Stars ilicheza michezo miwili ya kujipima nguvu kuelekea michuano hiyo mikali zaidi Afrika, mchezo wa kwanza dhidi ya Misri ilipoteza kwa goli 1-0 na kutoa sare ya 1-1 dhidi ya Zimbabwe.

Michezo hiyo imekuwa sehemu nzuri kwa timu hiyo kuelekea michuano hiyo ambayo walifuzu kwa mara ya kwanza tangu miaka 39 iliyopita baada ya kuifunga timu ya Taifa ya Uganda.

Timu hiyo iliondoka wiki iliyopita kuelekea Misri ambapo maandalizi ya michuano hiyo yamekamilika huku mchezo wa ufunguzi ukiwa Misri dhidi ya Zimbabwe Ijumaa saa nne usiku.

MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba na mabingwa ...

foto
Mwandishi: Rahimu Fadhili

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi