loader
Picha

Simba SC yaitambia Gwambina FC

TIMU ya Daraja la Kwanza ya Gwambina FC imeshindwa kutamba mbele ya Simba baada ya kufungwa kwa penalti 4-2 baada ya kutoka sare ya kufunga bao 1-1 katika mchezo wa kirafi ki uliofanyika kwenye Uwanja mpya wa Gwambina uliopo Misungwi mkoani Mwanza.

Mashabiki mbalimbali walifurika kushuhudia mtanange huo uliowakutanisha mabingwa wa Lgi Kuu soka Tanzania Bara pamoja na timu hiyo ya Daraja la Pili.

Gwambina FC wanajiandaa kwa Ligi Daraja la Kwanza iko katika michuano ya ligi daraja la Kwanza imeendelea kujifua kujiandaa na msimu ujao wa ligi hiyo Mchezo huo ulianza kwa timu zote kuoneshana ufundi kwa kupelekeana mashambulizi ya hapa na pale na mnamo dakika ya 24 mwamuzi ludovick Charles alimuonesha kadi ya njano mchezaji wa Simba, Said Ndemla baada ya kumfanyia madhambi mchezaji wa Gwambina Yusuph Kagoma.

Anuar Jabir aliifungia Gwambina bao la kuongoza katika dakika ya 50 baada ya kutokea piganikupige katika lango la Simba. Simba walisawazisha katika dakika ya 85 kwa bao lililofungwa na Said Ndemla.

Awali kabla ya mchezo huo ifanyika ibada ya shukrani iliyoongozwa na Padri Nzungu wa Parokia ya Tarazo Mwanza na kuhudhuriwa na wananchi mbalimbali iliyofanyika katika viwanja hivyo vya Gwambina. Mkurugenzi wa timu ya Gwambina Alexander Mnyeti alisema mpaka Sasa uwanja huo umekamilika kwa asilimia 85 na hadi kufikia Octoba utakuwa umekamilika kwa asilimia 100.

Alieleza kuwa mpaka Sasa uwanja huo umefikia asilimia 85 ukiwa umetumis Milioni 838 na unatarajia kukamilika kwa asilimia 100 Penalti za Simba zilifungwa na Ndemla, Hasan Dilunga, Yusuf Mlipili na Ben Jacob wakati Gwambina waliofunga Yussuf Mfaume na Salaga Mbido.

WAWAKILISHI wa Tanzania katika michuano ya Kombe la Shirikisho, Afrika ...

foto
Mwandishi: Yasinta Amos, Misungwi

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi