loader
Picha

Mimba za utotoni tishio Lindi

MIMBA za utotoni zimekuwa tishio mkoani Lindi na tangu Januari hadi mwezi huu, wanafunzi 60 walishapata ujauzito kutoka shule za sekondari na msingi mwaka huu.

Mkuu mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi alisema hayo kwa nyakati tofauti katika Halmashauri za Wilaya ya Kilwa na Lindi jana wakati alipokuwa akizungumza na madiwani wa Halmashauri ya Lindi.

Alisema hali ni mbaya mno, wanafunzi wanapata ujauzito na wengine kukimbiwa na familia zao. Alisema Wilaya ya Lindi kuna wanafunzi tisa wa shule ya msingi na sekondari waliokuwa wamepata mimba hadi mwezi huu na wanafunzi wawili wa shule ya msingi wa miaka 13 walipata ujauzito darasa la tatu Kilwa.

Alisema mazingira ya mimba yanaashiria wazi kuna muungano kati ya watendaji na wazazi kwani aliyempa mimba mwanafunzi hakamatwi na hakuna ushirikiano na vyombo vya serikali, vijiji na wazazi. “Jambo la muhimu sasa ni bora kuwakamata watendaji wa vijiji, hadi mwenyekiti, wazazi wote na kuhakikisha aliyempa mtoto ujauzito, yaani wote wakamatwe,” alisema.

Zambi alisema bila hivyo kila siku wataimba bila mafanikio kwani mtu anayempa mimba mwanafunzi anakimbia au yuko hapo hapo kijijini bila ya kukamatwa na binti anatoroshwa na wazazi wake.

Alisema Wilaya ya Kilwa pekee yake kuna wanafunzi wapatao 33 waliopata ujauzito na mtoto mwingine alikimbiziwa wilayani Kibiti mkoani Pwani na babu yake na kufanyishwa mapenzi mkoani Pwani. Zambi alisema pia mwanafunzi wa shule moja ya msingi mwenye umri wa miaka 13 alipewa ujauzito na mtu mzima kama baba yake au babu wakati serikali inapiga kelele au kukemea mwingine anaharibu.

KATIKA kuendeleza Sayansi, Teknolojia na Ubunifu nchini , umefanyika utafiti ...

foto
Mwandishi: Kennedy Kisula, Lindi

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi