loader
Picha

Mkurugenzi Tamwa apewa tuzo

MKURUGENZI wa Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (Tamwa), Rose Reuben (pichani) ametwaa Tuzo ya Wanawake katika uongozi iliyotolewa na World Women Leaders Congress (WWLC) jijini Dar es Salaam juzi.

Tuzo hizo zilitolewa kwa wanawake viongozi wa Afrika Mashariki walioleta mabadiliko katika jamii, walioibua vipaji, wanawake mifano ya kuigwa na wenye uthubutu kutoka taasisi na mashirika mbali mbali ya binafsi na serikali kutoka katika ukanda wa Afrika Mashariki. Wanawake viongozi kutoka Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi walitunukiwa tuzo hizo kutokana na vigezo vya ushindi vilivyowekwa.

Akizungumzia tuzo hiyo, Reuben alisema tuzo hiyo inawatia moyo wanawake wengine kufanya bidii zaidi kwani kuna watu wanawakubali na wanaweza kuzitunuku kazi zao. “Wanawake wanaweza kuwa viongozi wazuri, tuzo hii inaeleza kuwa uongozi wa wanawake unakubalika, hii ni tuzo ya dunia, kumbe ulimwengu umekubali kuwa wanawake wanaweza kuwa viongozi,” alisema.

Aliongeza: “Jamii kwa ujumla ikubali kuwa wanawake wanaweza kuwa viongozi. Wanahabari wafanye kazi zao kwa kujiamini, kazi zao zikajulikana na wasikatisshwe tamaa na kitu chochote.” Wengine waliotwaa tuzo hizo kutoka Tanzania ni Mkurugenzi Mtendaji na Mwanzilishi wa Taasisi ya Maofisa Watendaji Wanawake Tanzania, Emma Kawawa.

Tuzo hizo zinatolewa ili kuhamasisha wanawake viongozi katika sekta za umma na binafsi, kutambua mafanikio ya wanawake kikanda na kidunia na kuwatia moyo wanawake vijana kushika nafasi za mbali mbali za uongozi.

TIMU ya Taifa ya Soka ‘Taifa Stars’ inatarajiwa kushuka dimbani ...

foto
Mwandishi: Vicky Kimaro

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi