loader
Picha

JKCI kushirikiana hospitali za mikoa magonjwa ya moyo

TAASISI ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) imeahidi kushirikiana na hospitali za mikoa ya Mtwara, Manyara na Tanga kwa kuwatuma wataalamu wake kwenda kutoa huduma za matibabu ya kibingwa ya moyo katika hospitali hizo ili kusogeza huduma karibu zaidi na wananchi.

Hayo yalisemwa hivi karibuni na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo, Profesa Mohamed Janabi wakati akizungumza na viongozi wa hospitali za mikoa ya Mtwara, Manyara na Tanga waliofanya ziara ya kikazi ya mafunzo ya siku tatu katika taasisi hiyo.

Profesa Janabi alisema ziara ya viongozi hao imewasaidia kujifunza na kujionea kwa macho huduma mbalimbali za matibabu ya moyo zinazotolewa kwa wagonjwa wanaotibiwa katika taasisi hiyo. “Tutakuja kuwatembela katika hospitali zenu, tutaona huduma mnazozitoa na tutashirikiana kwa pamoja kutoa huduma kwa wananchi. Taasisi yetu imekuwa ikienda katika hospitali mbalimbali za mikoa kutoa huduma za matibabu ya moyo kwa wananchi kwa siku za mbeleni nanyi mtakuwa miongoni mwenu,” alisema.

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya mkoa wa Manyara, Dk Catherine Magali aliishukuru taasisi hiyo kwa kuwapokea na kuwapongeza kwa huduma bora wanazozitoa kwa wagonjwa wanaowatibu. Dk Magali alisema katika ziara hiyo wamejifunza jinsi ya kuwajibika na kutoa huduma nzuri kwa mgonjwa hata kama mtoa huduma halipwi chochote.

“Kuwepo kwetu kwa siku tatu katika taasisi hii tumejifunza na kujionea jinsi mgonjwa anavyopokelewa, kwenda kulipia bili, kwenda kwa daktari, kufanyiwa vipimo na kupewa dawa kwa wakati hakuna kuchelewa katika kupata huduma. Nasi tutaenda kuyafanyia kazi haya tuliyoyaona katika hospitali zetu,” alisema.

Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Tiba Shirikishi wa Taasisi hiyo, Dk Delila Kimambo aliwashauri viongozi hao kuzingatia usafi katika hospitali zao na kuhakikisha huduma bora zinatolewa kwa wagonjwa kwani hakuna mtu ambaye anapenda kulipia huduma mbaya.

Dk Delila alimalizia kwa kuwasihi viongozi hao kuvitunza vizuri vifaa vya hospitali zikiwemo mashine zinavyotolewa na wafadhili ili ziweze kutumika muda mrefu kwa kutoa huduma kwa wagonjwa. Katika ziara yao ya mafunzo ya siku tatu viongozi hao wa hospitali za Manyara, Tanga na Mtwara walitembelea maeneo mbalimbali ya Taasisi hiyo na kuona huduma za matibabu ya moyo zinazotolewa.

TIMU ya Taifa ya Soka ‘Taifa Stars’ inatarajiwa kushuka dimbani ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Maalumu

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi