loader
Picha

Kocha Misri atamba kuendeleza furaha

KOCHA Mkuu wa timu ya soka ya Misri,Javier Aguirre amesema anataka kuendelea kuwapa furaha mashabiki wao wa nyumbani kwa kushinda kila mechi. Aguirre amesema hayo baada ya kuibuka na ushinidi wa bao 1-0 katika mechi ya ufunguzi dhidi ya Zimbabwe juzi wa Kombe la Mataifa ya Afrika.

“Tunataka kuwapa furaha mashabiki wetu, ndio maana nilifanya maamuzi kwenye kikosi na mambo yamekwenda kama tulivyopanga,” alisema.

Hata hivyo, Misri haikuonyesha soka la kiushindani katika mechi hiyo, lakini kocha wake amesema ilikuwa mechi ya kwanza kila mchezaji alitaka kushinda mbele ya mashabiki wa nyumbani na ndio maana hawakucheza kama ilivyotarajiwa.

“Lakini mipango yetu yote imekwenda sawa, tunajiapanga na mechi ya pili na tunaamini itakuwa nzuri zaidi.”

Kwa upande wa kocha wa Zimbabwe, Sunday Chidzambwa alisema wamekuwa kwenye kiwango kizuri tangu walipoanza maandalizi ya michuano hiyo na kwenye mechi yao ya ufunguzi imedhihirika hilo.

“Tangu tumeanza maandalizi yetu tumekuwa tukicheza vizuri na leo (juzi) kila mmoja wetu aliliona hilo, wakati mwingine matokeo mazuri ni bahati, lakini wachezaji wangu hawakuniangusha,” alisema.

Misri sasa inaongoza Kundi A ikiwa na pointi tatu, ikisubiri matokeo ya mechi nyingine ya kundi hilo kati ya Uganda na Congo DR iliyotarajiwa kuchezwa jana jioni.

NYOTA wa klabu ya Arsenal inayoshiriki Ligi Kuu ya England, ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu, Cairo

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi