loader
Picha

Wachezaji Cameroon wasitisha mgomo

KIKOSI cha timu ya taifa ya Cameroon hatimaye kiliondoka Yaounde kwenda katika mashindano ya Mataifa ya Afrika, Afcon 2019, juzi Ijumaa baada ya kumaliza mgomo wa kudai kungezewa bonasi waliyoahidiwa.

Bonasi hiyo inahusu na kushiriki mashindano hayo makubwa kabisa barani Afrika.

Wakielekea Misri wakiwa na Simba hao wasiofungika, aziri wa Michezo Narcisse Mouelle Kombi aliandika katika ukurasa wake wa Facebook, alitupia picha akiwa pamoja na wachezaji wa timu hiyo kwenye Kiwanja cha Ndege cha Younde.

Wachezaji hao Alhamisi waligoma kuingia ndani ya ndege kwa ajili ya kwenda Misri kushiriki mashindano hayo ya Afcon.

Baada ya mgomo huo, Kombi aliendesha kikao cha usiku wa maneno na baadhi ya wachezaji wakongwe wa kikosi hicho na wawakilishi wao ambako viongozi wa Shirikisho la Soka la Afrika (Fecafoot) walikubali kuongeza kiasi cha euro 7,600 (sawa na sh milioni 20).

Wakati wakipewa kiasi hicho cha fedha, tayari kila mchezaji wa Cameroon alikuwa amepewa euro 30 489 (sawa na sh milioni 77) na serikali ya nchi yao.

Cameroon ambao ni mabingwa watetezi wa Afcon, awali ndio walitakiwa kuandaa fainali hizo za mwaka huu, kabla ya kupokonywa kutokana na kushindwa kukamilisha maandalizi kwa wakati.

Cameroon itaanza kutetea taji lake kwa kucheza dhidi ya Guinea-Bissau Jumanne, katika kundi hilo la F,

NYOTA wa klabu ya Arsenal inayoshiriki Ligi Kuu ya England, ...

foto
Mwandishi: CAIRO, Misri

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi