loader
Picha

Waliopisha miradi ya umeme kulipwa

WANANCHI waliopisha miradi mikubwa ya umeme kwenye mikoa ya Pwani, Dar es Salaam na Dodoma watalipwa fi dia wakati wowote baada ya uhakiki kukamilika.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu alipokuwa akizungumza na wananchi wa mtaa wa vitendo, alipokuwa akizindua uwashaji umeme.

Mgalu amesema, limechukua muda mrefu kutokana na uhakiki na fedha hizo zisingeweza kutolewa haraka, kwani wengine walikuwa wakitaka kujinufaisha kupitia malipo hayo.

“Tunaomba samahani kwa kuchelewesha fidia kwani tunajua baadhi wanasubiri tangu mwaka 2013 lakini kulihitajika umakini sana ili kuepuka upigaji,” alisema Mgalu.

Alitaja maeneo hayo kuwa ni njia za Rufiji Chalinze, Dar es Salaam hadi Chalinze na Chalinze hadi Dodoma, ambapo wanatarajia kukutana na wananchi wanaohusika na jambo hilo.

“Wananchi waliopitiwa na miradi hiyo watalipwa hakuna atakayenyimwa haki yake kikubwa ni kuwa na subira tu kwani wajibu wa serikali kufanya hivyo,” alisema Mgalu.

Aidha, alisema kuwa lengo la serikali ni kuhakikisha miundombinu, inawafikia wananchi ili ibaki kupeleka umeme majumbani.

“Tanesco sasa nao watakuwa na miradi ya kuunganisha umeme kwa maeneo ulikopita umeme mkubwa ili kila mtu apate huduma ya umeme,” alisema Mgalu.

Mwakilishi wa Meneja wa Tanesco Mkoa wa Pwani, Kenneth Boimanda alisema kuwa kaya zote ambazo ziko kwenye eneo la mradi zote zitapatiwa umeme.

Boimanda alisema kuwa nyumba zote wataalamu, watapita kukagua eneo lote la mradi ili umeme uweze kuwafikia wananchi.

Mbunge wa Kibaha Mjini, Silvestry Koka alisema kuwa wakandarasi wahakikishe wanawafikia wananchi wote ili kuondoa malalamiko.

Koka alisema pia wananchi wana jukumu la kulinda miundombinu ya umeme.

TIMU ya Taifa ya Soka ‘Taifa Stars’ inatarajiwa kushuka dimbani ...

foto
Mwandishi: John Gagarini, Kibaha

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi