loader
Picha

RPC asiyekomesha ukatili kuwajibishwa

MKUU Jeshi la Polisi nchini (IGP), Simon Sirro amewaagiza makamanda wa polisi wa mikoa yote, kupambana na ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto ili kukomesha matukio hayo.

Sirro pia amesema kamwe hatamvumilia askari yeyote, atakayeshindwa kulisimamia suala hilo.

Amesema atamwajibisha askari wakiwemo wakuu wa polisi wa mikoa, watakaoshindwa kusimamia suala hilo kikamilifu.

Akizungumza wakati wa mkutano uliolenga kujadili masuala mbalimbali ya kukabiliana na vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa watoto, ulioandaliwa na Shirika la Utu wa Mtoto (CDF) na kuwahusisha makamanda wa polisi kutoka mikoa mbalimbali, Sirro alisema hatua hiyo pamoja na mambo mengine itawawezesha wasimamizi hao wa usalama nchini kuwa makini dhidi ya matukio ya ukatili.

Amesema katika kukabiliana na matukio mbalimbali ya kikatili, jeshi hilo limekuwa likitumia mbinu mbalimbali ikiwemo ya kuanzisha dawati ya kushughulikia vitendo vya ukatili wa kijinsia ili kutoa chachu kwa wananchi hususani wahanga kwenda, hivyo ili waweze kwenda kutoa taarifa zao juu ya aina ya ukatili waliofanyiwa.

Aliongeza kuwa katika kuhakikisha suala hilo linakwenda kikamilifu, Polisi imekuwa ikishirikiana na wadau wakiwemo CDF katika kuwafikia waathirika wa vitendo na kuwachukulia hatua wahusika, ikiwemo kuwafikisha katika vyombo vya sheria.

TIMU ya Taifa ya Soka ‘Taifa Stars’ inatarajiwa kushuka dimbani ...

foto
Mwandishi: Oscar Job

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi