loader
Picha

Majukwaa TSN yawezesha wananchi kuelewa fursa

WAKUU wa Mikoa ya Tabora na Geita, wamesema Jukwaa la Fursa za Biashara lililofanywa na Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) katika mikoa yao, limesaidia kuwajengea wananchi na wawekezaji uelewa kuhusu fursa za biashara na uwekezaji katika mikoa hiyo.

Katika Mkoa wa Geita, jukwaa hilo la fursa za biashara na uwekezaji lilifanyika mwezi Agosti 2018 wakati mkoani Tabora lilifanyika mwezi Novemba 2018.

Wakizungumza na gazeti hili, wakuu wa mikoa ya Tabora, Aggrey Mwanr na wa Geita, Robert Gabriel, walisema kuwa moja ya matokeo makubwa ya jukwaa hilo ni kuongezeka kwa uelewa wa wananchi kuhusu fursa za biashara zilizomo kwenye mikoa yao pamoja na uelewa kwa wawekezaji kuhusu fursa hizo.

Mwanri amesema kupitia jukwaa hilo la fursa za biashara na uwekezaji, kuna kampuni moja ya Kichina imeonesha nia ya kutaka kufanya uwekezaji wa pamoja na mwananchi mmoja mzawa wa mkoa huo kwenye ujenzi wa kiwanda cha kuzalisha mafuta ya alizeti.

Amesema kiwanda hicho, kinatarajiwa kuanza kufanya kazi mwezi Aprili 2020 na kinachoendelea kwa sasa ni taratibu za kupata hati miliki.

Amesema kuwa asilimia 50 ya ardhi ambayo ilikuwa hailimwi, hivi sasa imeanza kutumika kwa kilimo cha mazao mbalimbali.

Mkuu wa Mkoa huyo amesema baada ya jukwaa hilo, wananchi wameelewa vizuri kuhusu suala ya uwekezaji na ujasiriamali ; na ndiyo maana Tabora ilishika nafasi ya pili kitaifa katika ugawaji wa vitambulisho vya wafanyabiashara wadogo maarufu ‘machinga’.

“Jukwaa limekuwa na manufaa makubwa kwa sababu limeongeza uelewa wa wananchi kuhusu fursa za biashara na uwekezaji zilizomo ndani ya mkoa huu, nitoe wito kwa wananchi wa Tabora warudi nyumbani kufungua biashara, viwanda na kujenga shule za kisasa, watambue kwamba fursa hazitolewi bali zinachukuliwa, hivyo waje wawekeze nyumbani,” alieleza Mwanri.

Alisema kutokana na jukwaa hilo, wameamua kutenga maeneo kadhaa kwa ajili ya biashara au uwekezaji fulani.

Alitaja baadhi ya maeneo hayo kuwa ni pamoja na wilaya ya Kaliua, ambako limetengwa eneo kwa ajili ya ranchi ya mifugo, viwanda vidogo vya mazao ya misitu na kiwanda cha mafuta ya karanga na alizeti.

Kwa upande wa Wilaya ya Sikonge, amesema kuna eneo limetengwa kwa ajili ya uwekezaji wa kiwanda cha kuchakata asili na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), iko tayari kutoa mikopo kupitia kitengo chao cha uwajibikaji wa kijamii (corporate social responsibility) kwa wanaotaka kuwekeza kwenye sekta hiyo.

Kwa mujibu wa Mwanri, kuna eneo limetengwa kwa ajili ya uwekezaji wa kiwanda cha nyama na machinjio ya kisasa Nzega, kwa kuwa mkoa huo una ng’ombe zaidi ya milioni mbili.

Alisema kupitia kiwanda hicho, wataweza kuuza ndani na nje ya nchi nyama, ngozi, pembe na samadi.

“Wilaya ya Urambo tumetenga eneo kwa ajili ya kiwanda cha kuchakata tumbaku, Uyui kiwanda cha chakula cha mifugo, Igunga na Nzega tumetenga maeneo kwa ajili ya kuanzisha ranchi ndogo kwa ajili ya kuboresha mifugo,”alisema Mwanri.

Mkuu wa Mkoa wa Geita, Robert Gabriel, amesema Jukwaa la Fursa za Biashara limesaidia kujenga sifa nzuri ya mkoa huo kwenye suala la biashara na uwekezaji, ambapo awali ulisifika kwa matukio mabaya ya mauaji na ushirikina.

Gabriel alisema uelewa wa wananchi kuhusu biashara ya madini, umeongezeka na ndiyo maana mkoa umeamua kufungua masoko mengi ya madini likiwemo Soko Kuu la Dhahabu Geita Mjini, Nyarugusu, Nyakagwe na Katoro na masoko mengine matano yalipangwa

Mkoa wa Pwani umebaini kuwa maonesho ya bidhaa zinazozalishwa viwandani ...

foto
Mwandishi: Matern Kayera

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi