loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Jela kwa kutumia ndizi kuiba benki

Mwanaume mkazi wa Bournemouth, Uingereza Laurence Vonderdell, 50, amehukumiwa kifungo cha miezi 14 jela kwa kuvamia benki na kuiba pesa  akitumia ndizi kama silaha.

Inadaiwa kuwa, hivi karibuni Vonderdell aliingia kwenye Benki ya Barclays na kwenda kwenye dirisha la kuweka na kutoa fedha na kisha kumweleza mhudumu ampatie fedha huku akiwa amemuoneshea ndizi iliyofunikwa na mfuko wa plastiki wa rangi ya machungwa.

Akidhani ni bastola iliyofunikwa na mfuko huo, mhudumu huyo alimpatia mwanaume huyo Euro 1100 ambayo ni sawa na milioni 2 laki nane na kisha mwanaume huyo akaondoka.

Ofisa wa Polisi wa eneo hilo Cos Andy Hale amesema, saa chache baada ya tukio hilo mwanaume huyo alikwenda kujisalimia kituo cha polisi na kueleza kuwa ameiba kwa kutumia ndizi, aliyoifanya kama bastola.

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi