loader
Picha

Taifa Stars yaanza vibaya Afcon

TANZANIA jana ilianza vibaya fainali za 32 za Mataifa ya Afrika baada ya kupokea kichapo cha mabao 2-0 kutoka kwa Senegal katika mchezo wa Kundi C uliofanyika jijii Alexandria, Misri.

Kipigo hicho sio tu kimefifisha nafasi ya Taifa Stars kucheza hatua ya 16 bora, lakini pia kimewakatisha tamaa Spika wa Bunge Job Nduga, wabunge wa Jamhuri na Watanzania kwa ujumla, ambao walikuwa na matumaini makubwa na timu yao kufanya vizuri, na walikuwepo uwanjani hapo.

Tanzania inashiriki mashindano hayo kwa mara ya kwanza baada ya miaka 39. Kwa mara ya mwisho Tanzania ilifuzu fainali hizo mwaka 1980 zilipofanyika Nigeria.

Katika mchezo huo uwa jana liofanyika kwenye Uwanja wa Juni 30 jijini Cairo, Misri, wachezaji wa Taifa Stars walishindwa kabisa kutamba baada ya kucheza chini ya kiwango na kuwaacha Senegal wakitamba.

Kipa Aishi Manula wa Tanzania, alijitahidi kuzuia michomo kibao ya Senegal iliyoelekezwa langoni mwake, na kuruhusu mabao hayo mawili licha ya Senegal kupeleka mashambulizi kibao.

Katika mchezo huo, Senegal ndio walikuwa wa kwanza kulifikia lango la Taifa Stars na Niang kukaribia kufunga katika dakika ya pili tangu kuanza kwa mchezo huo, lakini alipiga shuti lilitua mikono mwa kipa Manula.

Senegal katika mchezo huo, waiandika bao la kuongoza katika dakika ya 28 lililofungwa na Keita Balde baada ya mabeki wa Taifa Stars kushindwa kuokoa na mfungaji kuujaza mpira wavuni. Senegal nusura wafunge tena katika dakika ya 31 wakati Sarr aliposhindwa kujaza mpira wavuni licha ya kuwa katika nafasi nzuri.

Awali, Niang katika dakika ya 27 Niang alipiga mpira wa adhabu na nusura afunge, lakini mpira huo uligonga ukuta wa wachezaji wa Taifa Stars na kurudi uwanjani.

Kwa matokeo hayo, Taifa Stars inashika mkia baada ya kucheza mchezo mmoja na kupoteza mmoja, huku timu ya Kenya, Harambee Stars ikitarajia kucheza baadae usiku jana na Algeria katika mchezo mwingine wa Kundi C.

Taifa Stars mchezo ujao itacheza dhidi ya Kenya Juni 27 kabla ya kuhitimisha mechi za makundi dhidi ya Algeria.

Hii ni mara ya 14 kwa timu ya taifa ya Senegal kucheza final hizo za Afcon wakati Tanzania inashiriki kwa mara ya pili baada ya kucheza kwa mara ya kwanza mwaka 1980, miaka 39 iliyopita wakati fainali hizo zilipigwa nchini Nigeria.

Pia kipigo hicho kinamaana kuwa, Tanzania imeshindwa kulipa kisasi kwa Senegal baada ya time hiyo kufugwa 4-0 katika mchezo wa kufuzu kwa Afcon katika mchezo wa kwanza uliofanyika nchini Senegal kabla ya timu hizo kurudiana na kufungana bao 1-1 timu hizo ziliporudiana CCM Kirumba jijini Mwanza 2007 wakati huo timu hiyo ikifundishwa na Mbrazil, Marcio Maximo.

Kikosi cha Taifa Stars kilichoanza; Aishi Manula, Kelvin Yondan, Aggrey Moris, Gadiel Michael, Hassan Ramadan, Mudathir Yahya, Feisal Salum, John Bocco, Mbwana Samatta na Simon Msuva.

Katika mchezo uliotangulia Morocco nusura ilazimishwe sare na Namibia baada ya Morocco kuibuka na ushindi wa mbao 1-0, ambalo walilipata baada ya Namibia kujifunga.

NYOTA wa klabu ya Arsenal inayoshiriki Ligi Kuu ya England, ...

foto
Mwandishi: Zena Chande, Cairo

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi