loader
Picha

Okwi aishika pabaya Simba

KIWANGO kizuri kilichooneshwa na mshambuliaji Emmanuel Okwi wa Uganda kwenye mechi ya michuano ya Kombe la Mataifa Afrika ‘Afcon’ mi wazi kimemfanya mchezaji huyo azidi kupanda bei na kuiweka pabaya Simba.

Okwi aliyemaliza mkataba wake kwa mabingwa wa Ligi Kuu Bara Simba, kwa sasa yupo mjini hapa na timu yake ya Taifa, Uganda Cranes na juzi alifunga bao moja kafika ushindi wa timu hiyo wa 2-0 dhidi ya DR Congo.

Mbali na kufunga bao hilo, Okwi aliibuka mchezaji Bora wa mechi hiyo na kukabidhiwa tuzo baada ya mchezo huo.

Okwi aliyemaliza Ligi Kuu msimu uliopita akiwa na mabao 16, juzi alionesha kiwango cha hali ya juu na kuwavutia mashabiki waliofika kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Cairo kushuhudia mechi hiyo ya Kundi A.

Simba haijamalizana na Okwi, kwani baada ya mkataba wake kumalizika alitaka apewe kiwango kikubwa cha fedha kwa ajili ya kuongeza mkataba mwingine, lakini mabingwa hao wa Tanzania Bara, hawakuwa tayari kumuongezea.

“Okwi kaondoka Dar na kila kitu chake akisema anataka kutafuta changamoto upya lakini akasema kama tukiwa tayari kukubali kiasi anachotoka tumwite tumalizane,” amesema kiongozi mmoja wa Simba ambaye hakutaka jina lake litajwe.

Ni wazi kuwa sasa Simba itabidi ifanye kazi ya ziada kumpata kama inahitaji huduma ya Mganda huyo.

TIMU ya soka ya Taifa, Taifa Stars juzi iliweka tena ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu, Cairo

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi