loader
Picha

Rais- Uzoefu umetubeba

RAIS wa Shirikisho la soka Uganda (Fufa), Moses Magogo amesema uzoefu ndio sababu kubwa ya kuifunga Congo (DR) katika mechi yake ya kwanza ya michuano ya Kombe la Mataifa Afrika, Afcon 2019.

Uganda juzi iliibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Congo na kuifanya iongoze Kundi A ikifuatiwa na mwenyeji Misri.

Akizungumza mjini hapa jana, Magogo alisema uzoefu wa kushiriki michuano ya mwaka 2017 Gabon uliibeba kwani wachezaji wengi ni walewale waliocheza michuano iliyopita.

“Ushindi wa jana (juzi) naona tulibebwa na uzoefu, lakini pia tulifanya maandalizi ya kutosha kwa timu yetu.”

Kuhusu mechi ijayo dhidi ya Zimbabwe, Magogo alisema anaamini kocha atakipanga vizuri kikosi chake kwani Zimbabwe si timu mbaya.

“Tuliiona ikicheza na Misri, ni timu nzuri sio mbaya, kocha atapanga vizuri timu yake tupate matokeo. “amesema.

NYOTA wa klabu ya Arsenal inayoshiriki Ligi Kuu ya England, ...

foto
Mwandishi: Zena Chande, Cairo

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi