loader
Picha

Mbunge- Wachezaji Taifa Stars wanapunjwa posho

Mbunge wa Mbozi Pachal Haonga (Chadema) ameomba mwongozo wa Kiti cha Spika kuhusu madai kuwa wachezaji wa timu ya soka taifa 'Taifa Stars' wanadai posho na huenda kuna mgomo wa kimya kimya.

Jana Senegal waliifunga Taifa Stars mabao 2-0 katika mchezo wa kwanza Kundi C kwenye Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) nchini Misri.

Haonga leo ameomba mwongozo bungeni kwa Naibu Spika Dk Tulia Ackson, akidai kuwa, kuna tetesi kwamba wachezaji wa timu hiyo walitakiwa kupewa posho ya dola za Marekani 300 kwa siku lakini sasa wanapewa Dola za Marekani 70.

“Kuna tetesi ambazo zinaendelea katika mitandao ya kijamii kwamba Serikali ingeweza kuwapatia wachezaji wa Taifa Stars dola za kimarekani 300 kwa siku kule Misri lakini taarifa zilizopo ni kwamba wanapewa dola 70 hivyo inaonekana hawajalipwa hela zao kama wanavyotakiwa kulipwa kila siku,” amesema.

Kwa mujibu wa Mbunge huyo, kuna mgomo wa kimya kimya Taifa Stars na kwamba kuna siku wachezaji waligoma kufanya mazoezi.

Alieleza kuwa anaamini katika michezo lazima suala la morali lipewe kipaumbele ili mchezaji acheze vizuri.

“Hali hii ndio ilisababisha siku moja wacheza kugoma kufanya mazoezi hivyo matokeo hayo ya jana huenda ni mgomo wa kimya kimya unaendelea,” amesema baada ya kipindi cha maswali na majibu.

Naibu Spika,Dk Ackson amesema hawezi kujibu jambo hilo kwa sababu halijatokea ndani ya Bunge.

“Waheshimiwa wabunge kanuni ya 68 fasihi ya saba inataka kiti kitoe mwongozo kwa jambo ambalo limetokea bungeni mapema, jambo hili halijatokea hapa bungeni,”amesema.

TIMU ya soka ya Taifa, Taifa Stars juzi iliweka tena ...

foto
Mwandishi: Halima Mlacha, Dodoma

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi