loader
Picha

Uganda yaibeba EAC Afcon

UGANDA imeibeba Afrika Mashariki kwenye michuano ya fainali za Kombe la Mataifa Afrika, Afcon 2019, baada ya kuwa timu pekee kutoka ukanda huo kushinda mchezo wake na kuondoka na pointi zote tatu.

Kwa mara ya kwanza ukanda wa Afrika Mashariki umetoa timu nne kwenye michuano ya Afrika mwaka huu, ambazo ni Tanzania, Uganda, Kenya na Burundi iliyofuzu kwa mara ya kwanza. Uganda iliyopo Kundi A, ilianza kampeni zake kwa kucheza na DR Congo na kuibuka na ushindi wa mabao 2-0.

Rais wa Shirikisho la Soka la Uganda, Moses Magogo alisema ushindi wao ni kutokana na uzoefu walioupata kwenye michuano ya Afcon iliyofanyika Gabon 2017.

“Uzoefu umetusaidia, kushiriki Afcon ya Gabon 2017 imekuwa faida kwa sababu wachezaji wengi walioshiriki michuano ile ndio pia wapo hapa (Misri), hivyo uzoefu umetusaidia kwa kiasi kikubwa,” alisema.

Wakati Uganda ikipeperusha vema bendera ya Afrika Mashariki, hali ilianza kuwa mbaya kwa Burundi iliyofungwa bao 1-0 na Nigeria.

Hata hivyo matokeo hayo yamepokewa kwa hisia tofauti na mashabiki wa soka wengi wakiipongeza Burundi kwa matokeo hayo wakiamini ni timu ndogo, lakini ilijitutumia dhidi ya Nigeria na kufungwa bao hilo moja.

Hali ilizidi kuwa mbaya kwa timu za Afrika Mashariki baada ya juzi Tanzania na Kenya zote kupoteza mechi zake kwenye uwanja wa June 30 mjini Cairo.

Tanzania ilikuwa ya kwanza kucheza na Senegal na kufungwa mabao 2-0 kabla Kenya haijafungwa idadi kama hiyo ya mabao dhidi ya Algeria.

Matokeo hayo yanaifanya mechi kati ya Stars na Kenya inayotarajiwa kufanyika Alhamisi kuwa ya vute ni kuvute, kwani sasa kila mmoja anataka kushinda.

NYOTA wa klabu ya Arsenal inayoshiriki Ligi Kuu ya England, ...

foto
Mwandishi: Zena Chande, Cairo

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi