loader
Picha

Mwakyembe- Taifa Stars ilipwaya kiungo

Tuzo Mapunda WAZIRI wa Habari,Utamaduni Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe amesema kupwaya sehemu ya kiungo kwenye kikosi cha timu ya soka ya Tanzania, Taifa Stars ni sababu iliyowafanya kupoteza mchezo wa awali dhidi ya Senegal kwa mabao 2-0.

Mchezo huo ulikuwa wa kwanza kikosi hicho kutupa karata yake dhidi ya Simba hao wa milima ya Teranga katika muendelezo wa fainali za Afcon zinazoendelea kupigwa nchini Misri kwenye fainali za Mataifa ya Afrika, Afcon 2019.

Kwa matokeo hayo yanawafanya Senegal kuendelea kuongoza kundi hilo wakiwa na hazina ya pointi tatu wakifuatiwa na Algeria wenye pointi kama hizo wakizipata baada ya kuwakandamiza Kenya kwa kichapo cha mabao 2-0.

Mwakyembe ametoa maoni hayo baada ya kuangalia mchezo huo uliokuwa unatazamwa na Watanzania wengi kote nchi wakiwa na matumaini ya kuona timu hiyo inapata matokeo chanya.

Mwakyembe amesema Stars wanapwaya sehemu kiungo kumewagharimu kwa kiasi kikubwa na kumtaka kocha Emmanuel Amunike kufanya maboresho kuhakikisha washambuliaji wa timu hiyo wanaoongozwa na Mbwana Samatta, waweze kutimiza majukumu yao ya kufunga.

“Wapinzani wetu wanaonekana wanafungika, kikubwa ni kurekebisha makosa ya kiungo na mwisho wa siku tunaweza kufikia malengo, mwalimu afanye maboresho haraka kuelekea kwenye mechi inayokuja.

“Kikosi chetu kimekosa muunganiko kutoka safu ya ulinzi, kati na sehemu ya mwisho ya kumalizia, lakini kitu kilichonikera wachezaji wakipata mpira wanarudisha nyuma,” amesema Mwakyembe.

Baada ya mchezo huo, Stars wanajipanga kwa mchezo wa pili kwenye Kundi C dhidi ya majirani zao Kenya mechi inayotarajiwa kuwa ngumu kwa pande zote kutokana na wawili hao kujuana.

NYOTA wa klabu ya Arsenal inayoshiriki Ligi Kuu ya England, ...

foto
Mwandishi: Tuzo Mapunda

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi