loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Halmashauri yapewa mwezi ipime na kuuza viwanja

HALMASHAURI ya Wilaya ya Chamwino imepewa mwezi mmoja kuhakikisha imepima viwanja na kuuza, ili kuongeza mapato ya ndani huku akitaka wafanyakazi kuwekewa utaratibu wa kuuziwa viwanja kwa bei nafuu.

Agizo hilo limetolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Selemani Jafo alipokuwa akizungumza na wafanyakazi wa halmashauri hiyo. Jafo ameendelea kusisitiza kuwa Mkurugenzi ambaye halmashauri yake itashindwa kutenga na kutoa asilimia 10 ya mapato ya ndani kwa watu wenye ulemavu, vijana na wanawake kwa mwaka wa fedha unaoishia Juni 30, mwaka huu, atatumbuliwa.

Alisema Chamwino ambayo ndio wilaya ilipo Ikulu, haitakiwi kuwa nyuma kimapato kwani wakitumia chanzo cha upimaji na uuzaji wa viwanja, halmashauri hiyo itaongeza ukusanyaji wa mapato ya ndani.

“Ninyi Ikulu iko kwenu, kwanini msipime maeneo yenu na kuuza, tena mnaweza kuuza kwa bei ambayo wananchi wanaweza kununua, kwa kufanya hivi mtakuwa mmeupanga mji wenu vizuri lakini pia mapato ya ndani ya taongezeka.”

Jafo aliagiza wapime na kuuza ndani ya mwezi mmoja hadi mwisho wa Julai na kwamba, wakichelewa wanaweza kujikuta mapato yakienda Halmashauri ya Jiji la Dodoma. Jafo pia alisema baada ya kukamilisha upimaji na uuzaji wa viwanja ni vyema wakatoa pia kipaumbele kwa wafanyakazi wa halmashauri hiyo ambao wanaweza kuuziwa kwa bei nafuu na kuwekewa utaratibu wa kulipa kidogo kidogo.

“Mkiwaweka wafanyakazi wenu kwenye mpango wa kupewa viwanja na kuwawekea utaratibu mzuri wa kulipa, mtawajengea kuwa na ari ya kufanya kazi, hivyo msiwaache wafanyakazi kwenye mpango wa viwanja,” alisema.

Aidha, alitumia fursa hiyo kumpongeza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Chamwino na uongozi wake kwa ujumla kwa kuhakikisha inatoa asilimia 10 ya mapato ya ndani kwa ajili ya wanawake, vijana na walemavu. Mwaka wa fedha 2018/2019 ni mwaka wa kwanza wa utekelezaji wa sheria iliyotungwa na Bunge ambayo inazilazimisha halmashauri zote nchini kutenga asilimia 10 ya mapato ya ndani na kutoa kwa vikundi vya vijana (asilimia 4), wanawake (asilimia 4) na watu wenye ulemavu (asilimia 2).

KAMPUNI ya uzalishaji wa vifaa mbalimbali vya umeme cha Kilimanjaro ...

foto
Mwandishi: Anastazia Anyimike, Dodoma

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi