loader
Picha

Uchumi wakua 8.4% ndani ya robo mwaka

TAKWIMU za Wizara ya Fedha na Uchumi inaonesha uchumi wa Rwanda umekua kwa asilimia 8.4 katika robo ya kwanza ya mwaka huu.

Katika miezi mitatu ya kwanza ya mwaka, Pato la Taifa la Ndani (GDP) kwa bidhaa na huduma za nchini humu linakadiriwa kuwa faranga bilioni 144 likiwa ni ongezeko kutoka faranga bilioni 1,987 zilizopatikana katika kipindi kama hicho mwaka jana. Waziri anayeshughulikia Mipango ya Uchumi katika wizara hiyo, Claudine Uwera, alisema uchumi unatarajia kuwa imara kutokana na kiwango cha ukuaji wake.

Kilimo, huduma na sekta ya viwanda zina mchango mkubwa katika ukuaji wa uchumi kwa utoaji huduma ikichangia kwa asilimia 48, kilimo asilimia 28, huku viwanda vikichangia kwa asilimia 17 ya ukuaji wa pato la taifa. Alisema asilimia saba zilizobaki zinatokana na kodi na ruzuku za bidhaa ambapo katika robo hiyo, kilimo kimekua kwa asilimia nne, viwanda asilimia 18, huku utoaji huduma asilimia nane.

Hata hivyo, usafirishaji wa mazao nje ya nchi umeshuka kwa asilimia tisa kutokana na kushuka kwa uzalishaji wa chai kwa asilimia saba pamoja na kushuka kwa asilimia 19 uzalishaji wa mazao ya biashara kama maua, miwa, pareto, huku uzalishaji wa kahawa ukiongezeka kwa asilimia mbili.

TIMU ya Taifa ya Soka ‘Taifa Stars’ inatarajiwa kushuka dimbani ...

foto
Mwandishi: KIGALI

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi