loader
Picha

Nyoni yupo fiti kuwakabili Wakenya

BEKI ya Taifa Stars, Erasto Nyoni amesema kwa sasa anaendelea vizuri, hivyo kama kocha Emmanuel Amunike atampanga mechi dhidi ya Kenya, Alhamisi, atacheza bila shida yoyote.

Nyoni yupo mjini hapa na Taifa Stars inayoshiriki michuano ya Afcon na juzi alishindwa kucheza mechi ya kwanza dhidi ya Senegal kutokana na kusumbuliwa nyama.

“Nina shida kidogo ya mguu, nyama zinanisumbua lakini nilishaanza mazoezi mepesi mechi ijayo naweza kucheza kocha akinipa nafasi,” alisema.

Kukosekana na Nyoni kuliipa Stars pengo kubwa katika nafasi ya ulinzi, jambo lililofanya Senegal kuipenya ngome ya Stars kirahisi na kuwa mzigo mkubwa kwa kipa Aishi Manula aliyelazimika kuokoa hatari kibao langoni mwake mara kwa mara.

Katika mechi hiyo, Stars ilifungwa mabao 2-0 na kujiweka kwenye mazingira magumu, kwani sasa italazimika kushinda mechi ijayo dhidi ya Kenya kama inataka kuweka hai matumaini ya kusonga mbele kwenye michuano hiyo.

Stars inatarajia kucheza na Kenya Alhamisi kwenye Uwanja wa June 30, jijini hapa.

WAWAKILISHI wa Tanzania katika michuano ya Kombe la Shirikisho, Afrika ...

foto
Mwandishi: Zena Chande, Cairo

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi