loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Serikali yapitisha mpango kukopa fedha za bajeti

SERIKALI inahitaji mkopo wa dola za Marekani milioni 500 kutoka benki za Afrika kukabiliana na upungufu wa fedha katika bajeti yake. Waziri wa Habari, Michael Makuei alisema mkopo huo utasaidia kukabiliana na upungufu wa pauni ya nchi hiyo bilioni 77.4 za bajeti.

Alisema fedha hizo zitatumika kwa mishahara, miundombinu, kilimo na mahitaji mengine muhimu na kuwa mkopo huo utalipwa kwa kipindi cha zaidi ya miaka minne. “Hatujafahamu mkataba utakuwa wa aina gani, pamoja na riba, lakini baraza la mawaziri limeshapitisha kuchukua mkopo huo,” alisema. Makuei alisema Waziri wa Fedha ameelekezwa kupeleka maombi ya mkopo bungeni ili kuidhinishwa.

Fedha ya serikali katika mwaka wa fedha 2019/2020 ni pauni za nchi hiyo bilioni 130.7 ambapo asilimia 77 inatarajiwa kutokana na mapato ya mafuta, huku asilimia 23 kutoka mapato mengine yasiyo ya mafuta.

Wakati huohuo, Michael Makuei amekiri kuwa Sudan Kusini imeshindwa kulipa ada katika Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kutokana na tatizo la kifedha. Sudan Kusini inatakiwa kulipa dola milioni nane katika EAC kila mwaka, lakini kutokana na matatizo ya kifedha wameshindwa kulipa na ndiyo sababu ya kutaka kuchukua mkopo huo.

MGOMBEA Urais wa Chama ...

foto
Mwandishi: JUBA

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi