loader
Picha

Magufuli- Kufungwa 2 na Senegal si mbaya

Rais John Magufuli amesema, wachezaji wa timu ya soka ya Taifa 'Taifa Stars' wasikate tamaa kwa kuwa kufungwa mabao 2-0 na Senegal si matokeo mabaya sana.

Ametoa mwito kwa Watanzania wawape moyo wachezaji wa Taifa Stars kwa kuwa kufungwa kwao ni kufungwa kwa Watanzania na kushinda kwao ni ushindi kwa Watanzania.

"Kwa hiyo wao wakakazane, wakajitume zaidi, na sisi tuendelee kuwaombea...kwa hiyo tusimame tuendelee kuwasaidia na kuwaombea"amesema akiwa Vijibweni wilayani Kigamboni, Dar es Salaam kwenye hafla ya uzinduzi wa maghala na mitambo ya gesi ya kampuni ya Taifa Gas.

"Na mimi nina uhakika huo mwanzo sio mbaya sana, kufungwa tugoli tuwili tu, kwa timu ambayo inaongoza katika Afrika, ambao wachezaji wote wale wanacheza nje, mimi nilifikiri tuendelee kuwapa moyo"amesema Magufuli.

Katika uzinduzi huo Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amemuhakikishia Rais Magufuli kuwa Taifa Stars itawafunga Kenya Juni 27 mwaka huu na akaomba ruhusa aende Misri.

"Bwana ninakuruhusu nenda, si umesema ukienda tutashinda basi nenda kwa sababu sisi wote tunataka kushinda. Kwa hiyo kapande ndege leo nenda na ukawaambie wachezaji wasikate tamaa. Kwenye uwanja wa mpira kuna kushinda na kushindwa. Kwa hiyo kama unaenda kule pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni nendeni wote, mkahakikishe tunashinda" amesema Rais.

WAWAKILISHI wa Tanzania katika michuano ya Kombe la Shirikisho, Afrika ...

foto
Mwandishi: Basil Msongo

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi